Monday, October 26, 2015

UNAWEZA KUIVUKA JANA YAKO NA KUENDELEA MBELE HATA KAMA INA MAUMIVU NA MACHOZI KIASI GANI!!!

UNAWEZA KUIVUKA JANA YAKO NA KUENDELEA MBELE HATA KAMA INA MAUMIVU NA MACHOZI KIASI GANI!!!

    Mara nyingi tunapokutana na mapito makali kwenye maisha huwa tunaona kabisa ni NGUMU /HAIWEZEKANI kuiona kesho au mbele yetu.Huwa ni wakati mgumu na usio rahisi sana,ila ni kipindi kinachohitaji.
√Muda
√Ujasiri
√Nguvu za kutosha na kubwa zaidi
√KUAMINI INAWEZEKANA KUENDELEA MBELE..
   *Kuna kukua sana unapopita kwenye mitihani na changamoto ile hali ya mwanzo ya kupaniki,kutetemeka huondoka maana unajua jambo hilohilo likitokea mara ya pili utalishinda vipi.Hata mtazamo wako juu ya mambo fulani utapanuka maana tunasema "matatizo ni kipimo cha AKILI"

*Kama matatizo yalikufanya ukakosa furaha baada ya kuyavuka una nafasi ya kuipata kwa viwango vikuu.
Pale ambapo unaamua kuchagua upande CHANYA kwamba haijalishi ninapita kwenye nini lazima nivuke ng'ambo..lazima nishinde..HAKIKA INAKUA HIVYO

1.CHAGUA SHUKRANI-mshukuru Mungu kwa yote unayopitia hata yawe yana ugumu na kuumiza kwa kiwango kikuu hii itakupa amani ya nafsi na kukupa nguvu za kusonga mbele.Si wewe pekee unayepitia hayo..je?yale mema uliyonayo uliyastahili..na haya mabaya ulipenda yampate nani?
Moyo wenye shukrani hupokea baraka maradufu..
Unapolipokea jambo na kulikabili badala ya kulificha na kulizika ni mwanga mzuri kisaikolojia maana itakupa kuiona mbele kwa urahisi

2.CHAGUA MAOMBI-maombi ni mawasiliano baina yako ni MUNGU kwa imani yoyote uliyonayo..kuna vitu ni Mungu pekee anao huu uwezo wa kutusahaulisha hata kuponya madonda kwenye moyo.Mweleze bila kuficha jambo moja baada ya jingine..Jifunue..funguka.ha ha ha kuna mambo yanaumizaaaa na huwezi mwambia mtu yoyote anaeweza tunza SIRI sasa Mungu hutunza mno mno.
mfanye rafiki yako mueleze ukiona unalia lia weeee mpaka uchungu ukome..Fanya hivyo mpaka moyo wako umepona hauna kisasi..haujihukumu..haujaandaa kisasi kwa yeyote..uko tayari kusonga mbele ndiposa utakua uko sawa.
Ila ukiona umeomba bado moyo unauma..unatamani kufanya baya kwa waliokukosea rudi tena kwa Mungu mpaka uwe sawa.

3.CHAGUA KUBADILI UELEKEO
             Tupa nyuma yote uliyopitia,yale yasiyokujenga au kukuhudumia..Yape kampani mapya yoteee yanayokupa kukua na kuendelea mbele.
JIPENDE...JIFURAHIE maana kuyavuka maumivu na mateso ya nyuma kwenye maisha yetu si rahisi na huchukua muda..ila ukiamua binafsi kwamba yatosha MWANGA HUONEKANA TU..
  Hata mimi nilipita na kwa haya machache nilivuka na ninasonga mbele.HATA WEWE UNAWEZA

NINAKUPENDA NA KUKUOMBEA CHOCHOTE CHA NYUMA KINACHOKUSONGA NA KUKUNYIMA KUENDELEA MBELE KIKUACHIE ILI UTIMIZE NDOTO ZAKO NA KUFURAHIA MAISHA ...

No comments:

Post a Comment