Tuesday, October 8, 2013

BINTI JASIRI KUTOKA PAKISTANI...........

Kutana na binti wa ki~Pakistani MALALA YOUSAFZAI binti jasiri aliyeteka hisia za ulimwengu kutokana na harakati zake kupigania haki za wanawake na hasa mabinti kuhusu kupata elimu..
            N 
MALALA binti aliyezaliwa  tarehe 12.7.1997 hukoMingora Pakistani jina lake likiwa na maana ya (GRIEF STRICKEN) Alijipatia umaarufu mwaka 2009 kupitia BBC pale alipoandika makala kuhusu Talibani na upinzani wao kuhusu mabinti kupewa elimu..jambo lililopelekea MALALA kushambuliwa na Talibani ndani ya basi akitoka shule  tarehe 9.10.2012 ambapo alipigwa risasi kichwani na shingoni...
  • MALALA~Akiwa hospitali ya QUEEN ELIZABETH alipopelekwa kwa matibabu.....
MALALA kwa sasa anahodhi tuzo mbili kama 1. NATIONAL YOUTH PEACE PRIZE ~2011  na SIMONE DE BEAUVOIR PRIZE~2013 ......Malala kwa sasa yuko Uingereza akiendelea na masomo yake huku akiwataka mabinti kutochezea fursa wanazopewa maana kwao Pakistani wanazililia fursa hzo............

2 comments: