Kwenye maisha kila mmoja huwa na maono ya kule anataka kufika au mtu gani anataka awe..Ukikaa na watoto wadogo watasema nataka niwe daktari,rubani,mwalimu nk.Kwa waliopita hiyo hatua watasema nataka kuwa rubani mwenye kuendesha madege makubwa kimataifa,niishi nyumba ya ghorofa au nataka kufika pale..
Si dhambi kuwa na ndoto,ni sawa kabisa lakini umeandaa mikakati kuzifikia.Wengi wetu tukiwa na ndoto tunatazama PESA kwanza..lakini bila mikakati thabiti hata ikiwa nyingi utagota pahala.
Unaandika wapi ndoto au maono uliyonayo?
Ni vizuri kuwa na kijisehemu spesheli kuweka maono na ndoto zako.Hii itakusaidia hata kuweka mikakati na kufanya mchanganuo na tathimini..umefanikiwa kiasi gani na hata uliposhindwa kipi kimekukwamisha.
kwa watumiaji wa simu za touch kwenye play store yako waweza download notebook na reminder ya kukusaidia kwenye mipango yako.
√NANI umshirikishe maono yako ni jambo la kuzingatia..Kwa wasomaji wa biblia mnafahamu hadithi ya Yusufu na nduguze pale alipowashirikisha maono yake..maana alipowambia tu nna anavyoona kesho yake alijipatia upinzani mkuu..Wewe je!una moyo wa kupambana?au laini ambao ukikatishwa tu tamaa unaacha ndoto zako..Ukishajijua uko upande upi,angalia mtu ambaye unamwamini na unajua atakupa mwongozo kuelekea ndoto zao..ILA kwa experience yangu binafsi jiandae kibinafsi utakapoiva waendee sasa waliopiga hatua wakupe ujuzi na hata ukikutana na wakukuvunja moyo usikate tamaa Tulia..Vuta pumzi..ingia kwenye internet jisomee then songa mbele..
√Kuna wakati utawakuta watu wanafanya kitu kama chako..WASIKUTISHE kila mtu aliyeumbwa na Mungu ana ladha yake tofauti..hivyo pambana na ushindani kwa kujiamini na kile ulichonacho wewe binafsi..
Haya mpendwa nenda katimize ndoto zako..
You can do it..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
This is great and Very empowering, My sister keep it going
ReplyDelete