Wednesday, January 15, 2014

Vijana na mahusiano!!!

Basi baada ya kuahidi nitawajuza baadhi ya mafundisho yaliyojiri kwenye ilee semina hapa chuoni UDSM...nikaona acha tuanzie hii ya mahusiano maana na mie blogger inanihusu si ndio enheeee..ila kama itakufaa na ukavaa shela au suti msininyime kadi nije nile ubwabwa na kudance hahaaaaaa..

Alisimama Mchungaji Christopher akasema title ni uchumba hadi ndoa ila mimi nitaanzia kwenye ndoa..hapo sasa tukainua macho na masikio kwa mwalimu kama anavyoonekana pichani>>>>


NDOA-ni wito wa kupendana na kutumikiana.
           -ni umoja na urafiki pasipo na unafiki..
           -sio tukio ni maisha...
           -ni muunganiko wa kiMungu na kisheria..
           -inahusisha kitendo cha mtu kuhama kimakazi,kihisia kutoka kwa wazazi na kwenda kuwa mwili mmoja..unahama kijiografia na kihisia kuwa sasa si wazazi tena wanaokufanyia maamuzi ila wewe unasimamia maisha yako mwenyewe wao wanabaki washauri tuu pale mnapokwama kabisa..sio unataka kununua kochi unafunga safari kagera kuwauliza wazazi..

Mungu anapaswa kuhusishwa kwa 100% na zaidi toka kipindi cha uchumba..

MAMBO YA MSINGI KWA KIJANA ANAYETAKA NDOA:
1. Tafakari makini~tumia muda mwingi kumtafuta Mungu na maongozi yake ,bila kusahau kuwa kati ya wanawake wengi au wanaume unaokutana nao mke/mme ni mmoja
2.Ukomavu wa kiroho~hapa alisisitiza kuwa mtu binafsi kutenga muda wa kumtafutaMungubila ya kusukumwa na mtu yoyote..akaendelea kusema ndoa si shati kwamba likibana utagawa.... hapa alisihi vijana kuwa makini kwani kuna changamoto za ndoa zinamhitaji Mungu sasa kama mwenzi wako ni
mchanga itakuwa balaa.
3.Ukomavu wa akili~angalia umri wako je,umepevuka kimaisha..utaweza kuhimili changamoto za ndoa au ukikutwa na mambo wewe ni kuangua kilio badala ya kuzitatua au unazikabidhi kwa wazazi..kama utataka ndoa hakikisha akili imekua..
4.Maandalizi ya msingi~hapa alilenga zaidi wavulana kuhakikisha una kazi ya mikono inayokupa kipato..
5.Ufahamu sahihi juu ya ndoa…
6.Maamuzi sahihi juu ya mtu unayetaka kumuoa/kuolewa nae..

Alimalizia kuhusu ZINAA&UASHERATI
akasoma andiko la Waebrania 13:4
akasema mahusiano yanayohusisha tendo la kujamiiana ni NDOA kwa hiyo huu unaofanyika pembeni ni uasherati na akaasa vijana tusiwe jamvi la wageni kwamba kila mtu lazima akae..
akasema zinaa inakimbiwa si kuifanyia mazungumzo na piaaaa tendo la kujamiiana lililo la kushiba au toshelevu ni la kwenye ndoa huku pembeni ni kujipunja tuuu.

Somo ndioo hilooo wadau wenye wachumba   marufuku kuonjaonja subirini huko honeymoon au kama hata mchumba huna acha mashaka mwenzi wako yupo anakuombea nawe endelea kumuombea siku mkikutana moyo wenyewe utasema na msisite kusimamia nasaha za pastor na blogger..

VERSES;
# Mithali 6:27,mathayo 5:37,wimbo ulio bora 5:1,mithali 18:22#

Love you all!!
Mjitunzeeeeeeeeer

2 comments:

  1. Dats super havin u on JESUS' PLATFORM doing marvellous stuffs 4 HIS GLORY kip it u girl!

    ReplyDelete