Wednesday, February 1, 2017

Simama,Futa machozi,Tazama vyema

SIMAMA
FUTA MACHOZI
TAZAMA VYEMA
WEWE NI SHUJAA
         Woow maneno haya ni ya wimbo mmojawapo wa Angel Benard niliyapenda sana!nikiamka,nikikaa nakutafakari uzuri wa kuwa kwenye sayari hii yenye hewa ya bure ni mibaraka tele,huwa nauinjoi sana!
Haya maneno yakiongezewa vitendo yana nguvu na umhimu sana.Maisha si siku zote hurudisha shukrani,kuna nyakati hutusonga na mambo yanayoleta machozi,kujiona duni au usiye thamani,kuchelewa safari ya mafanikio au hata kupoteza yale uliyohitaji na kuyapa umhimu.Ila haijalishi bado nafasi ipo,kwenye changamoto zozote katu usipoteze T3
•Tumaini
•Tabasamu
•Tegemeo kwa Mungu

    Baada ya sarakasi zoote kwenye jambo lolote
SIMAMA :-hapa weka breki zote,acha pupa,hasira,majuto,acha kutafuta wa kumlaumu au kumtupia lawama,pekua nini kimekufikisha hapo?utakapopata jawabu itakusaidia sana kusonga mbele!

FUTA MACHOZI:-Hapa kabiliana na maumivu yako ya hilo lililokufika si kukwepa au kukataa kwamba umesongwa la hasha hapa kama ni kulia lia wee ila ukiwa umedhamiria kuinuka na kusonga mbele,waweza pata marafiki wema au familia itakayosimama nawe lakini hapa ni kukubaliana na ukweli kwamba mwisho wa siku wewe ndiye rubani wa maisha yako hao wote watapita, maana hata jengo hushikiliwa na machuma wakati wa ujenzi ila baada ya muda uondolewa na jengo hubaki pekee,hapa nina maana kuwa maisha ni WEWE jikung'ute mavumbi na aamua kutoka ndani kusonga mbele!

TAZAMA VYEMA:-Baada ya machozi kufutika naamini macho yataona vyema,zile fursa zilizo mbele yako hapa utagundua pia nini unakikosa kwa kuendelea kukaa kwenye uchungu na kukata tamaa,utaona pia namna unavyopoteza muda kujinung'unikia na kulaumu wengine!Hapa ni kipindi cha kuwa jasiri na kufanya maamuzi yatakayobadili maisha yako kwa mlengo chanya,

Wewe ni shujaa katika lolote unalokabiliana nalo daima jivike jina hili!hili litakupunguzia unyonge na kuwa mtu wa kulialia kila linapotokea gumu na zito

Chukua hatua yote unayotamani yanawezekana hasa na Mungu akiwa upande wako!
Praying for you❤️🙏🏿

No comments:

Post a Comment