BEAUTIFUL SINGLE CHRISTIAN GIRLS!
Heri ya mwaka mpya warembo!ngoja tufungue mwaka kwa kuongelea hili.
Imekuwa kawaida sana kwa mabinti kupata mafundisho ya kujitunza mpaka ndoa na hasa kutokana na madhara kuwa makubwa na mengi kwa upande wetu!ila kuna katabia kama kanaota mizizi kwa baadhi ya kujitengenezea mazingira ya vijana wa kiume kuwahitaji kingono halafu ikishafika point of no return,mnawaruka kimanga na kuwasingizia kuwa wametaka kuwaangusha dhambini nk. Nk.
Nadhani kama umeamua kujitunza fanya huku ukimlinda na huyo kijana mwenzio ila kumtega naye akanasa, halafu baadaye unatuaminisha kwamba ulilazimishwa nae si sawa!Huwa naamini binti wa kike ndiye mwenye dira ya uhusiano mlionao kama mjitunze mpaka ndoa au la,
Yasome mazingira yanayoongoza mahusiano yenu,msome na yeye madhaifu na nguvu zake (strenghth &weakness) na nyote msaidiane kuifikia NDOA TAKATIFU sio afya sana kuchochea moto usioivisha chochote!
- Jaribu kurekebisha namna unavyovaa mnapokuwa mnahitaji kuonana,valia kwa staha na si kwa namna ya kutuma ujumbe ambao baadaye utashindwa kuujibu itapobidi kufanya hivyo.
- Jaribu kuangalia mazingira ya hivyo vikao vyenu vya dharura!
Ni sawa kuwa binti mwenye misimamo!ila iwe yenye usafi na adabu,sio kumtia kijana wa watu kwenye vishawishi halafu baadaye unamruka!
No comments:
Post a Comment