HATUA 5 ZA KUJIKUBALI(Self acceptance)
Ni watu wachache sana ambao hujitahidi kujikubali kutokana na sababu mbalimbali.
■Mambo waliyokutana nayo maishani. mfano:-Mtu aliyepitia udhalilishaji wa kihisia,kinjisia,kuteswa,kubakwa/kulawitiwa,ubaguzi wa rangi nk . Huyu atapata shida kidogo au sana vile atakavyojitazama na kujichukulia kibinafsi.Wengi hudhani wao ni duni au hawakua na nguvu za kujipigania na kujitetea ndio maana wakayapitia hayo.
■Malezi:- Namna tunavyokua kwenye familia zetu hasa hizi za kiafrika Mara nyingi watoto hushushwa na kuonwa hawana upeo au jitihada kama fulani.Inauma pale mtoto anapoleta matokeo nyumbani akifeli atatukanwa na kufananishwa akili yake na mnyama au kuambiwa mbona mtoto wa fulani amefaulu wewe umeshindwaje?
■Haiba(Personality):-watu wenye kujidharau na kutokujibali wakati mwingine ni vile tu mtu alivyozaliwa kila wakati atawaona wengine ni bora kuliko yeye,atajiona duni tu hata ale nini,avae nini,afanyiwe nini bado kwake atajiweka duni tu..
Ufanye nini ukijikuta una hali hii au ungependa kumuinua yeyote mwenye hali hii:-
1. Acha kujizungumza hasi kukuhusu au kama ni mzazi au mume acha kumzungumza hasi mtoto/mkeo.Maneno yana nguvu..yanaumba wasomaji wa biblia watanielewa uzuri hapa "ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo" pia "mtu huvuna matunda ya kinywa chake"..acha kabisa kujidharau unaua asili ya ukuu na uwezo ulioko ndani yako.Watu wote unaowaona wamefanya vitu vinavyokuvutia walijizungumzia mema hata wengine walipowaona si kitu walijiamini na kusonga mbele.
Tafuta kioo nenda mbele yake kila leo jizungumzie..jitazame..jiite jina lako mfano:- Woinde wewe ni shujaa..wewe ni mrembo..hata hili unaliweza.. ukifanya hivi kuna kitu kinaumbika ndani utashangaa ujasiri huoo..kujipenda hukooo unaanza kufanya mambo yanakua..
Hata wengine wakikuona duni..wakikukosoa wakiona unacheka..unawapuuza na kuwa imara hawarudii ng'oo.
2. Jitahidi na jizuie kujilinganisha na wengine. Hakuna kitu kinanyonya nguvu na kualika huzuni kama kujilinganisha na mtu.Mungu alikua na maana yake kutuumba tofauti..hebu tuzipokee tofauti zetu kwa shukrani maana dunia ingeboa sana kama sote tungefanana.ukipita hapa unakutana na mtu mweusi,pale mweupe,mara huyu mfupi..kidogo tolu anaingia..Haya hata kwenye baraka kila mtu analo fungu lake..
Ridhika jinsi ulivyo na ulichonacho unachotamani kiongezee juhudi na maarifa ondoa "mbona mimi hivi..mbona yule ana hiki nk
3.Tunza mapungufu yako na historia yako huku ukiamini si wewe tu pekee uliyo nayo au uliyopitia hayo.Ni kweli una mapungufu lakini si ufurahie basi jitihada ulizowekeza kwenye kuyashinda.Kwenye maisha tunapita kwenye vingiii na kadri tunavyopiga hatua yale mabaya hutukimbiza nyuma..hutupigia kelele sana..hutakiwi kusimama na kujadiliana nayo maadam yalipita yamepita unayo haki yooote yakuendelea mbele kwa furaha na nguvu mpya.Ni kweli ulibakwa huna haja ya kulibeba hilo kovu na kujihukumu. .samehe..jipende..endelea mbele.
4.Tambua chanzo sahihi cha ujasiri wako..kama ni kumuomba Mungu..kufanya vile uvipendavyo..kusoma vitabu..kuzungumza na wanaokuamini na kukutia moyo nk yafanye yote hayo kwa nguvu zako zote.
5.Muache Mungu pekee akuthaminishe..Kamwe wanadamu hawawezi kutupa thamani ile ambayo tunayo machoni pa Mungu. Uwiiii Mungu anatupenda sana mimi nikipataga picha vile Mungu ananipenda..ananithamini na kunijali hujiona kama katoto kadogoo kanakobebwa au kuachwa kwenye chumba kilichojaa pipi..Ni utamu usioelezeka.
Hata wanadamu woooooooteeeeee wakuone kinyago..wakuteme mate..wakushushe chini jua na liweke moyoni na akilini kwamba MUNGU ANANIPENDA
MUNGU ANANIJALI
ANANITHAMINI
ANANIHESHIMU
mnooooooo mimi ni wa thamani kubwa mbele zake hilo litakupa hatua mpyaaa.
Wapenzi ngoja niishie hapa..
Mungu akupe kujikubali. .ishi maisha ya shukrani.wewe ni wewe dunia nzima hayupo kama wewe na hatotokea..maneno yoote yaliyokuvunja moyo.vitendo vyovyote vilivyokuharibu ufahamu kukuhusu vipuuze..chukua hatua mpya..jipende..jilishe..jitunze.TIMIZA ndoto zako..
Unataka ushauri na msaada zaidi
0718 664 741
Nakupenda na kukuombea..wewe ni wa thamani na gharama mnoo♥♥♡♡♡♡
No comments:
Post a Comment