Tuesday, November 10, 2015

Young Girls njooni tuongee

YOUNG GIRL'S!YOUNG GIRL'S nini kimewakuta?
Maisha gani haya mliyochagua?
Kipaumbele kwenye maisha yenu ni hiki kweli?
Ishu ni hii sayansi na teknolojia au?
Kwanini mmekuwa rahisi hivi?
   

     Mara nyingi sana mtoto wa kike ni kiumbe wa thamani na hufananishwa na ua la waridi lenye kunukia sana. Ua la waridi huvutia..hupendeza..hutamanisha mnoo ila ili lizidi kustawi huitaji matunzo.mbolea na maji ya kutosha.Sifa nyingine ya ua hili ni kuwa lina miiba mpaka umelichuma inabidi uwe mwangalifu kweli..Nadhani hata bei yake iko juu kuliko maua mengine yooote..
    Binti wa kike wewe ni kama hili ua wewe ni wa gharama,thamani ,pekee ,tofauti nk.
Ila nini kimewapata mabinti kizazi hiki mbona mmekuwa rahisi hivi. ?binti kaka akikutamkia amekupenda unachanganyikiwa jumla jumla unachukua nafasi yake wewe ndio unaanza kumtoa outing,kumlipia kodi,kuacha hata kuishi kwa wazazi wako na kuhamia kwake bila kujali unasoma au la.

Nani amekudanganya ili kumdumisha na kumumiliki mwanaume ni kumpa mwili wako?/kuhamia kwake?/kumtunza na kumhudumia kipesa?

Enhee unapoyafanya haya unaifikiria kweli kesho yako?ndoto zako unaziheshimu kweli?unafikiri kwa maisha haya utazifikia kweli?

Unajua tofauti ya upendo na tamaa?mtu anayekupenda unajua ana sifa zipi.?

●Jitunze...heshimu maisha na ndoto zako..heshimu vile wazazi wako wamejitoa kwa ajili yako na kujinyima ili ufike hapo ulipo..malipo gani haya unayowalipa..hivi wanajua hiki unachokifanya nyuma ya mgongo wao?hivi pesa yao wanajua inamnyooshea maisha kijana mmoja wa kiume hb huku town..
Heshimu mwili wako si kila anayekwambia anakupenda lazima umpe mwili wako kama Shukrani. .utawapa wangapi?mwanaume anayekupenda na kukuheshimu hawezi kukuvua nguo na kukuchezea atajali ndoto zako na kuhakikisha unajitunza mpaka wakati mwafaka

●Kipaumbele chako kwenye maisha ni kipi?ni mapenzi tu?una hakika?upo shule?naamini lengo ni kupambana  kuwa mtu fulani hapo baadaye SASA JE mbona unahama kwenye lengo?mapenzi si yapo tu..mtaka yote kwa pupa hukosa yote..Chagua moja wekeza nguvu zako zote hayo ya ziada yatakuja tu kwa wakati..Tumia ulichonacho kwa Shukrani kuna mabinti rika lako wanatamani shule hawana uwezo huo kwanini wewe unaichezea?

Hili ua la waridi huwaga linanyauka na kukauka kau..na watu tunasahau
Ubinti ni kipindi tuu kinapita unakua mke..unakua mama baadaye uzee huu hapa sasa kama unautumia ubinti wako vibaya unajiandalia majuto utabaki kuwatamani wenzio walioutumia vizuri kwa kujitunza na kutimiza ndoto zao.
Cherish your season. .kitendee haki kipindi chako cha ubinti..kuwa gharama. .pendeza..kuwa busy na shule na ndoto zako..mapenzi yapo tuu..wanaume wa nguvu wazuriiii wanazaliwa na wapo tu..ila kila kitu kiende kwa utaratibu
Acha wao ndio wapigane vikumbo kukutafuta mtoto mzuri. .bana miguu yako vizuri mpaka wakati muafaka hata kama ulishachezewa saana hujachelewa unaposoma makala hii unaweza kubadilika na kuwa mtoto mzuri..

Mwanaume anayekupenda anayejua wewe ni ua atakutunza..atafanya matunzo yooote stahiki ukishakomaa ndipo atakuchuma..

Usijirahisishe binti..utandawazi usikubadilishe kina telemundo..Marichui ...Angelo na Yna wasikudanganye pale ni tamthilia tuu wenzio wameandikiwa script yale ni maigizo yanarudiwa hata mara kumi ili kupata kipande kizuri cha kurushwa kwa television. Yale si maisha halisi hebu ishi maisha ya KiTanzania ambayo unayajua kama binti huku ukimuomba Mungu akutunze na kukusaidia.

Binti amka..Jitunze. .Jipende..Jijali..Ishi na timiza ndoto zako..

Penda nyinyi saana. .

No comments:

Post a Comment