Ukizungumzia wanawake ma role model huwezi kuacha kumtaja Joyce Meyer.Mwanamama huyu amekuwa chachu yetu mabinti kutokana na personality yake ambayo ni very strong na ni mtu ambaye ulimwengu unamtambua kwa mafundisho yake mbalimbali.
√ Joyce amezaliwa tarehe 4.6.1943 huko St.Louis Missouri Marekani, na jina lake lilikuwa Pauline Joyce Hutchuson.
√Joyce ni mwalimu wa biblia, mwandishi wa vitabu na mzungumzaji (speaker).
√Joyce ni mke halali wa bwana Dave waliyeoana naye mwaka 1967 na miaka yao kwenye ndoa ni 47 yenye baraka ya uzao wa watoto wa 4.
√Joyce hakuwa na makuzi mazuri utotoni alitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono na babaye mzazi .
√Joyce aliolewa kabla ya kukutana na Dave mmewe wa sasa ndoa iliyodumu miaka 5 iliyokuwa imejaa mateso kama vile uneending cheating za huyo mwanaume na alimshawishi Joyce aibe pesa kazini kitu kilichomuumiza sana Joyce na alirudisha pesa zote baada ya divorce.
love story ya Joyce na Dave ilianza baada ya Dave kutoka jeshini wakati akipita na gari yake akamwona Joyce aliyevalia pensi fupi akiosha gari lake na Dave akamwambia "" dada samahani unaweza kuosha na langu?"Joyce akamjibu'buddy if you want your car washed,wash it yourself'.
°Hakikua kitu kirahisi kwa Joyce maana alikua ndio kwanza ametoka kutalikiana na ndoa yake ya miaka mitano na pia ana kumbukumbu mbaya za sexual abuse kutoka kwa babaye.Anasema ilichukua muda kukubali ombi la Dave,hakuwaamini tena wanaume.Hata hivyo baadaye alikubali wakaoana.
*Anasema kilichomsaidia ndoa yake kufikia miaka 47 ni kumpata Dave mwanaume mcha Mungu aliyeweza kuchukuliana na madhaifu yake maana alikuwa mwanamke mwenye uchungu sana na alikuwa akiumia kwakuwa alikuwa na vituko vyote lakini Dave alikua akimvumilia.
*Joyce anasema kitu anachokikumbuka wakizozana na Dave ni kuhusu golf,kwani hakikuwa kitu anachokipenda na Dave alipenda sana ilimchukua muda kupenda na kujoin.
*Anasema siri kubwa ya kubadilika ni kulisoma sana neno la MUNGU kwani kulimpa yeye nafasi ya kuufaidi upendo wa MUNGU kibinafsi na ulimfundisha JINSI YA KUMTII mumewe licha ya kuwa ni mwanamke mwenye personality strong sana,anasema hajawahi kumtawala mumewe Dave na ni neno la MUNGU lililomfunza kunyenyea mamlaka na aliona authority ya kwanza kuwa submissive kwayo ni mumewe DAVE..
No comments:
Post a Comment