Rose Mushi ni dada wa kikristo mwenye influence kubwa kwa vijana aliyejikita haswa kwenye mafundisho yanayolenga kuwajenga,kuimarisha vijana kwa maisha ya sasa na ya baadaye kwa kifupi ni role model wa mabinti wengi kutokana na anavyoplan mambo yake na kuyafanya.
√Rose Mushi ni binti aliyeokoka na amezaliwa 30May miaka kadhaa iliyopita.
√Amesoma Ashira Girls na baadaye University of Dar Es Salaam alipotwaa digrii ya masuala ya uchumi,akiwa chuoni alikuwa kiongozi wa TAFES na muimbaji wa kundi la Annointed girls.
√Baadaye aliamua kutoa muda wake kufanya shughuli zake kwa vijana hasa mabinti kama muanzilishi wa Ladies of Destiny Network ambayo imelenga kuwajengea mabinti kujiamini, kujitambua,kujithamini.Na kupitia network hii amesomesha mabinti wengi na kuwasaidia.
√Rose ni mwandishi pia wa vitabu na ameandika karibu vitabu 16 kama "what makes a lady attractive,15 types of ladies in a dating world,why you should wait na vingine vingi lengo likiwa kuwapa taarifa sahihi vijana za kuwasaidia ili wafike wanakokutaka.
√Rose ni binti mwenye bidii asiyekata tamaa na daima amekuwa ni mwenye msimamo kwenye kile anachokifanya na moja ya kauli zake kwenye mafundisho yake "ladies your pants and bras should not be the desks upon which your cheques is signed"hapo akisisitiza mabinti kujitunza.
√Siku moja nilipata fursa ya kuongea nae na akasema kinachompa UJASIRI kuyasema hayo ni maisha yake binafsi kwani kama binti amejitunza na haruhusu kuchezewa na awaye yeyote.Anamshukuru Mungu ameweza kusomesha baadhi ya watu na moja ya watu anaomshukuru Mungu sana ni kijana aliyemsaidia kwa pocket money yake na sasa yuko chuo kikuu akisomea udaktari.,anapoona hayo anafarijika though anasema bado hajafika anakotaka na anajiona bado sana.
#kama wanawake tunajivunia wewe,,umekua mfano wa kuigwa keep it up...
No comments:
Post a Comment