Kutunza ujana, ndoa, uzee au wokovu wako ni
wajibu wa mtu mwenyewe. Ni kweli Mungu
anatutunza na anayosememu kubwa katika kila rika la maisha yetu; lakini amempa
mwanadamu ufahamu na utashi na anao wajibu wa kufanya ili kujitunza.
Ili kuutunza ujana wako ni lazima ujue na
uyazingatie mambo muhimu yafuatayo:
1.
NIZIJUE CHANGAMOTO ZINAZO
NIKABILI KIJANA
i)
Kwenda na Wakati–Biblia
inaagiza kuukomboa wakati-Waefeso 5:15-16
Ni changamoto kwetu na
ni fursa kutumia nguvu ya msalama kuishinda hii
kawaida ya Dunia
hususani vijana kuvutwa katika kwenda na wakati. Kijana huvutwa na kushawishika kwenda sawa na
wakati katika maeneo mengi. Kijana
anavutwa na kuvaa, kusuka, kunyoa, kutembea, kusema, kutenda sawa na wakati,
hata kumiliki vitu vinavyoendana na kuendana na wakati. Dunia inavyotuvuta
katika kwenda na wakati, Biblia inatuagiza kuukomboa wakati. Kuukomboa wakati ni kutumia vizuri wakati
tuliopewa kama fursa ya pekee. Wakati wa
Ujana ni wa kuwekeza vitu vya rohoni na mwili, komboa wakati.
a)
Komboa wakati Ki-Elimu: Usipoteze wakati kwa
mambo yasiyokuhusu, mfano kijana mwanafunzi Soma kwa bidii ni wakati wake, siku
ikiisha jiulize umeongeza nini ki-elimu? Usiishi kiholeholela tu fursa hiyo
inapita.
b)
Komboa wakati Ki-Uchumi: Usipoteze wakati kwa
matumizi ya kipuuzi, fasheni za mavazi, mitindo ya nywele, hata kijiko huna,
wewe unavaa tu. Komboa wakati ukijua kuna kuoa na kuolewa lazima ujipange
mapema. Siku ikiisha, wiki, mwezi, mwaka Jiulize umeongeza nini kiuchumi? Kumbuka kuna miaka saba ya shibe na miaka
saba ya njaa lazima uishi kwa adabu/hekima, siku zijazo huna nguvu ya kuwekeza
kama UJANANI.
c)
Komboa wakati Kiroho: Usipoteze wakati Kiroho,
tumia fursa hii vizuri. Siku inapoisha, wiki, mwezi, mwaka, kijana jiulize
umeongeza nini Kiroho. Umeongeza nini
ufahamu katika Neno la Mungu, Umeongeza nini Maombi, Umeongeza nini utumishi
wako wakati huu una nguvu, usiishi kiholela. Wekeza vitu vya Ki-Mungu ndani
yako, funga na kuomba, soma neno, tumika kadri uwezavyo. Ukifika uhitaji
yamkini hata huwezi kuomba sana unaakiba ya kutosha ya Maombi/Neno la kusimamia
kupita kipindi hicho.
d) Komboa wakati-tumia vizuri fursa ya kuwa kijana - 1Nyakat
12:32 Kwa
kufanya mambo yakupasayo kufanya wakati huu (ujanani) kila eneo. Wakati ujao ukifika hata ukitaka kurudi
darasani akili haitunzi tena
kumbukumbu kama leo na majukum yataongezeka, ukitaka kubeba zege huwezi huna nguvu kama leo, Kiroho vivyo hivyo, ukisoma
neno ufahamu unachoka haraka, kufunga
huwezi tena. Uwe na akili zijue nyakati.
ii)
Tamaa za Ujanani – 2Tim
2:22, Mith 27:2, 1Kor 6:18a, Wimbo 3:5
Ni changamoto kwetu na
ni fursa kuonesha nguvu ya msalaba kutiisha mwili.
Kijana anavutwa sana na
tamaa za ujanani na hizi zinamkumba kijana si kwa sababu hayuko kiroho hapana,
zinamkumba kwa vile ni kijana. Changamoto
hii tunaipata wote, vijana waliookoka na wasiookoka ila tofauti yetu ni katika
kuzi-hundle Kijana aliyeokoka anazitiisha na asiyeokoka anazitii tamaa hizi.
Biblia imetaja moja kwa moja kuwa ni tamaa za ujanani na
zinawakumba vijana wote na lazima kuzitiisha zisubiri wakati [NDOA].
Ni muhimu kuyajua, kuyaelewa na kuzingatia mambo 4
yafuatayo:-
a) Uhai wa milango ya
fahamu kwa kijana ni tofauti na rika nyinginezo.
Milango ya fahamu ni
Macho, Maskio, Pua, Mdomo, Ngozi-inauhai [active].
b) Uhai wa hisia za mwili
kwa kijana ni tofauti na rika nyingine. Unatokana na mabadiliko ya mwili
yaliwekwa na Mungu mwenyewe.
c) Upo Uhusiano wa karibu
kati ya Hisia za mwili wa kijana na Tamaa za ujanani, hili lazima kijana alijue
ili ajilinde.
d) a, b, na c hapo juu, zinatusaidia kujua sababu ya Mungu
kutuagiza watu Kukimbia tamaa za
Ujanani, tusichochee mapenzi mpaka Ndoa.
§ Inaagiza kwa msisitizo
kusema zikimbieni tamaa za ujanani/mwili.
Tumeongea na vijana wengi walioanguka hawakupanga kuzini. Ila wamezembea
katika kulitii Neno la Mungu badala ya kukimbia wao wanakaa, wanaleta hoja,
wanakemea, wanaomba, wanapinga mwisho wa siku wanajikuta chini, kwa ukaidi wao
kwa Neno la Mungu. Biblia haikushindwa kusema kemea, ombea, pinga ila imesema
KIMBIA.
§ Usichochee mapenzi,
usizichochee hisia za mwili/matakwa ya mwili.
Ø Milango ya fahamu ikichochewa inazalisha hisia katika mwili;
Ø Hisia/Msisimko wa Mwili wa kijana ukichochewa unazalisha uhitaji;
Ø Uhitaji wa Kimapenzi ukichochewa unazalisha Tamaa za Mwili;
Ø Tamaa za Mwili/Ujanani zenye msukumo mkali kutaka kukidhi
uhitaji zikichochewa zinalet anguko, mauti; Kijana hatua hii hakumbuki wokovu, huduma,
aibu, magonjwa yanayotokana na zinaa-Kaswende, kisonono wala Ukimwi. Hakumbuki
mimba au watoto wasiotarajiwa. Anahaha kutaka kukidhi uhitaji wa mfalme/malkia
wake tu, ni hatari.
Ø Mauti inazaliwa kutokana na Tamaa iliyopembejewa na Kijana. Kuna
Kijana alizilea hatua tulizojifunza hapo juu, hakuchukua hatua za Kiroho
kuutiisha mwili akajikuta anabaka-wadada na wakaka wote wanabaka japo hapo
tunamuona kaka amebaka – 2SAMWELI 13:1-22. Biblia inasema wazi unaingamiza nafsi
yako mwenyewe-Mithali 6:32.
Kuyalea na Kuyachekea
mambo hayo juu ndipo unaskia anguko, Kijana anayeheshimiwa na Mungu na watu
anajikuta amezini. Unapokosa subra
na kuparamia unalala na mke au mume wa mtu kiuumbaji.
Kimsingi kila mtu ameumbiwa mume au mke wake – Mwanzo 2:22.
iii) Vichocheo vya mapenzi/tamaa za ujanani/tamaa za mwili
Ni changamoto ya tatu
inayotukabili vijana na lazima tuishinde ili tusalimike. Ni muhimu kujua
vichocheo vya mapenzi/tamaa za mwili ili kuviepuka. Nisipojua vichocheo hivi si kiroho bali
ni ujinga unaotishia usalama wangu.
Vichocheo vifuatavyo huyaamsha mapenzi, huchochea tamaa za
mwili:-
a)
Kuzitafakari/kusikilizia
hisia za mwili-Inahusisha ufahamu wenyewe
Biblia imetuagiza tuyatafakari
yaliyo juu-Wafilip 4:8. Mungu alijua tukiyatafakari ya chini yakiwemo tamaa za
mwili tutachochea mapenzi.
§ Usijiulize maswali ya
kipuuzi mf. ‘Hivi, tafika kuoa au kuolewa bila kuonja? Wenzio walioonja
wamekuwa watumwa wa dhambi hiyo kujitoa ni gharama kubwa wengi wameshindwa
kuilipa, usiwaze kuonja hadi NDOA.
§ Baridi imezidi/Upweke jamani
niko peke yangu. Ulitaka uwe na nani? Haya ni majira ya Bwana yenye kusudi
timilifu uwe peke yako, wakati wa kuwa 2 na 12 watakapokuja hao wa kike na wa
kiume-utakuja tu, vumilia.
b)
Kusoma makala za mapenzi
[makala za Internet, magazeti, vipeperushi, vitabu]-inahusisha macho yanayosoma
makala.
§ Unashangaa binti au kaka
anasoma vitabu vya tendo la ndoa/Mapenzi.
§ Internet Café anaenda
kutazama mambo ya Ngono/Mapenzi. n.k.
Kijana huyu
atakuwa salama kweli au ndio hao mwisho anabaka mtu.
c)
Kutazama mambo ya ngono
au yanayohusu ngono-inahusisha macho.
Mikanda ya x, sinema za
x, picha za x hasa kwa internet na hata ‘live’ kuna watu wanapenda kuchungulia
sehemu zenye upenyo wa kufanya hivyo.
Raha yake aone tu utupu wa watu na mchezo unavyokwenda, atapona?
d)
Kushika au kushikana/kugusana-inahusisha
ngozi-Wakolosai 2:21.
§ Mkono unaganda dk.5 dada
na kaka wanasalimiana salamu yetu.
Mkono wako una chapa ya
Yesu usiruhusu kujinajisi kwa kutii mwili.
§ Vidole vinaongea kwa kupapasa
au kubonyeza au kutekenya ni uchochezi.
Vidole vyako vinachapa
ya Yesu, usiruhusu kujinajisi kwa mambo hayo.
§ Tongue Kiss/Denda ni hatari wala mtu
asijifariji kuwa salama-usionje.
Ulimi wako unachapa ya
Yesu usionje uchafu[mate] subiri Ndoa utanyonya mpaka uchoke ukitaka maana
utakuwa huru katika hayo si leo.
§ Ngozi ikiskia umeshika/kwa, unapapasa/swa, umekula denda, lazima itashtuka na
kuleta hisia ya kuvutwa katika ngono kwavile wewe ni kijana. Usiidhalilishe Chapa
ya damu ya Yesu uliogongwa siku ulipookoka, itunze.
e) Kusikiliza mambo/maneno ya ngono au yanayohusu ngono-sikio.
Sikio lako linachapa ya
Yesu usilisikizishe uchafu wowote-ni kichocheo.
Kusikia ni sikio kupata
jambo bila kukusudia lakin kusikiliza ni kukusudia. Hata kama sikio limenasa
uchafu kwa bahati mbaya hakikisha unalitoa.
f)
Kuongea mambo ya ngono
au yanayohusu ngono-inahusisha mdomo.
§ Mazungumzo ya Mdomo ni hatari-Mithali 6:26; 7:16-18,21. Iko nguvu katika
midomo/maneno. Biblia inasema Maneno huzaa uhitaji na sura hiyo hiyo ya 6,
inashauri jiepushe na midomo ya malaya; Kwa maneno alimshinda-si kwa mtutu, si
kwa ‘hug’ wala busu ni maneno tu na akamshinda. Usiruhusu kupokea maneno hata ya mzaha kuhusu ngono.
§ Mawasiliano katika Simu ni vema kuangalia sana unavyoenenda.
Idadi ya “Call au Sms” mfano kutwa mara tatu
unampokea Fulani.
Simu inazidi
‘dose’ ya Panadol kutwa mara tatu yeye mara tano. !!!!!
Muda wa “Call au Sms” mfano usiku sana au
alfajiri ni kichocheo.
Usiruhusu Simu za usiku
wa manane/alfajiri hata kwa manadai ya kuamsha ktk maombi kwa muda huo ataamsha
na vingine si maombi tena!
Sauti ya “Call” kuna sauti za uchochezi mfano kulegeza, kuguna, kutetemesha
sauti, sauti kama analia na nyinginezo kwa kijana utajua tu.
§ Mazungumzo “Simu au Sms” yakihusu ngono ni uchochezi sana.
Mambo hayo juu hata kama
mtu hajaweka neno la kimapenzi/kimahaba ni kichocheo, Je, mazungumzo yenyewe
hayo ni hatari zaidi mara 100.
Biblia inaonya
mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema-1Kor
15:33.
Mfano: Naskia baridi
njoo basi unipe joto, wewe umekuwa ‘heater’?
Najiona mpweke ‘lonelyness’ afadhali uje hapa
nichangamke. Kweli wewe una Baba, Mwana na Roho Mtakatifu bado mpweke?
Ukiyachekea hayo, hutaki
kuyakemea, anaongeza ‘dose’ sasa utaambiwa wazi zaidi ‘nina nyege, ni wewe wa
kutoa nyege zangu’
g)
Zawadi ni moja kati ya
vichocheo vya mapenzi kwa namna hii.
§ Size ya zawadi - Ukubwa, zawadi ya thamani kubwa. Itaua msimamo.
§ Idadi ya zawadi - Wingi vitu tele unapokea au mara nyingi-utalipa
tu.
§ Aina ya zawadi - Kitu gani unapokea-chupi? Zawadi hiyo itaongea
tu.
Msimamo wa Semina hii ni USITOE NA USIPOKEE ZAWADI. Tunaishi zama za uovu, usanii na malaghai mpaka Kanisani wa kike/kiume wao wanajua
kuipaka asali nia yao ili usishtuke mapema mpaka umefika chini, zawadi ni
chambo kukunasa we. Hutaki Kanuni hii yatakayo kupata usilie.
Wachumba: Vijana hawa wako huru kutoa/kupokea zawadi ila Kanuni ni hizo
hizo hapo juu. Uchumba si Ndoa muda huo bado unaendelea kumthibitisha Mungu,
usijeishia njiani ukalilia mtu na vitu
vyako.
h) Picha na Mikao ya Picha kwa jinsia mbili ni Kichocheo cha
Mapenzi.
§ Picha za nusu uchi eg.
Kifua/Tumbo/Mapaja wazi au chupi/sidiri tu.
§ Picha za utupu [mwili
wote], picha hii hana nguo hata moja-ni kichocheo.
§ Picha na Mikao yake
inavunja miiko ya jinsi ya kuenenda Vijana waaminio.
‘Pouse’ la Kushikana
Mabegani, Kushikana Viuno, Kushikana Kifua mtu anajikuta ameshika matiti katika
pouse la picha, Kushikana Makalio, Kubusiana Shavu au Mdomo, Kupakatana/Kukumbatiana
ni KICHOCHEO. Kijana usikubali Kuidhalilisha Chapa ya Yesu kwa Pouse la Picha.
i) Mavazi ya Vijana wa Kike na Kiume yanavyokuwa Kichocheo.
§ Mavazi ya Kuonesha Nguo za Ndani-Milegezo,Vifungo
wazi,Mipasuo n.k.
§ Mavazi ya Kuonesha Maungo/Maumbile-Kubana sana inachora
umbile, Kuangaza [transparent] inaonesha viungo vyote japo kavaa, ni vichocheo.
§ Mavazi ya Kutositiri Mwili-Nguo fupi-pensi/bukta/skert/gauni/blaus,
Nguo hizi huacha Kifua wazi, matiti nje, Kitovu nje, Tumbo nje, Kiuno nje,
Kwapa nje-ndio unakuta kijana haabudu anachungulia titi kupitia kwapa.
§ Ni maombi yetu mavazi hayo yasivaliwe nawe unayesoma makala
hii. Ni maombi yetu uushinde mwili, endapo
utakutana na mavazi hayo kazini, shuleni, kwenye daladala, barabarani,
dukani, sokoni na hata Kanisani kwa Waongofu Wapya au Wakongwe wenye mitazamo
tofauti. Utaona hatuwezi kuepuka hili moja kwa moja kwa jamii yetu ila tumejifunza
ili ukiona mavazi hayo usi-‘take
advantage’, usikodolee macho mpaka mate yanatoka huna habari ni hatari kwa
afya yako, epuka.
j) Mazingira hatarishi/njia kuu ni Kichocheo - Mithali 7:7-13a,
21-23.
Njia Kuu ni mahali pa
Kificho, Gizani, Uchochoroni, Chumbani, Ufukweni, Kuwepo wawili tu mnataka kufa
maana mazingira tu ni kichocheo tosha.
Kabla ya kugusana,
mabusu, zawadi, mazungumzo vyote hivyo bado, ile kuwa wawili tu maeneo hayo ni
kichocheo tosha na kinaongea kwa kasi.
Kijana mmoja mjinga yeye
alizubaazubaa NJIA KUU yaliyomkuta ni balaa.
Tunapomalizia kichocheo
cha 10 cha mapenzi hebu tusome andiko hilo.
Kijana huyu alitembea
muda hatarishi kwa kijana, akakaa mahali hatarishi, akakutana na mtu hatarishi
[kahaba], akaambiwa maneno hatarishi, akanaswa. Mithali 6; inatoaushauri kuwa
jiepushe na maneno ya Malaya n.k. ndipo sura ya 7; inaonesha kwa maneno ya ubembelezi
tu kahaba akamshinda Kijana kiulaini kabisa akaongoza njia kama Ng’ombe
aendavyo machinjioni uhitaji umeshapamba moto, mfalme amesimamisha majeshi hayarudi
chini, anaona nikidhi tu uhitaji wa mfalme nisalimike, kumbe maskini
anaiangamiza nafsi yake ya thamani-Marko
8:34-35.
Tunaishi zama za uovu
makahaba wa kike/kiume wapo Kanisani pia.
Makahaba hupenda NJIA KUU soma Ezekiel
16:22-26. Ni mahodari wa ubembelezi, kwa kiroho cha kusuasua cha
kutozingatia mipaka ya uhuru wetu, hutoki, utalainika mwenyewe na utajikuta
unaongoza njia kama kijana mjinga. Epuka mazingira hatarishi, kuna kisa
kilitokea Kanisani mkesha wa Vijana wa Maombi ya masaa 48. Kaka kamfata dada
anamwambia “nina nyege na wewe ndio wa kutoa nyege zangu” Ikiwa mkesha wa
maombi kuna watu wanamawazo hayo, je, huko njia kuu?
Umejua vichocheo 10, usichochee. Ukifanya uzembe
umenaswa hatua No.1 Mlango wa fahamu umepokea taarifa-Itoe mapema, ikiwa uko
hatua No.2 ya hisia/msisimko wa mwili pambana-usipembejee, kama ni hatua No.3
ya uhitaji usimridhie mfalme/malkia tiisha hali hiyo, usifikie hatua No.4 ya kuwaka tamaa ni mbaya sana inapelekea hatua
No.5 ya MAUTI.
2.
NIJUE JINSI YA
KUZIKABILI CHANGAMOTO KWA MUJIBU WA BIBLIA
Tumeona Changamoto 3
katika Somo hili, Kwenda na Wakati, Tamaa za Ujanani na Vichocheo. Hizi ni changamoto kali
kwetu ukitumia akili utachemsha. Ufuatao ni muongozo kidogo tu wa kukabiliana
na Changamoto hizo kwa mujibu wa Biblia:
i) Maombi-Uwe na maisha ya
maombi, ombea ujana wako siku zote-Luk 18:1;
Tabia ng’ang’anizi Funga na Kuomba na utapata
upako wa kuutiisha mwili.
ii) Neno la Mungu likae kwa
wingi ndani yako ili usafishe njia zako-Zab 119:9.
iii) Nikubali na niamue kwa
dhati kuusulubisha mwili/kuunyima matakwa yake.
§ Utu wa kale ni wakati
mwili ulipokuwa na nguvu, ukiokoka-Rum 6:6;12:1
Kama utu wa kale
unakung’ang’ani jichunguze pengine hujauvua vizuri- funga na kuomba utoke-Math
17:21. Umvae Kristo-Rumi 13:13-14.
§ Kuishi kinyume na mwili
na tamaa zake na mawazo yake-Galatia 5:24.
§ Paulo aliamua kutesa
mwili, wewe na mimi je?–1Kor 9:27; Marko 8:34-35;
Ukitaka kuiponya nafsi
ati mwili unahaha, mfalme amesimamisha majeshi au malkia anahaha acha niiponye
nafsi yangu kwa kukidhi uhitaji huu, maskini unaingamiza nafsi yako wala
huiponyi kama unavyodhani. Na ukiamua kuiangamiza nafsi yako kwa ajili ya
Kristo UNAIPONYA. AMEN.
iv) Nijitenge na ubaya wa
kila namna yaani ubaya wote-1Thesalonike 5:22.
Tangu
mwanzo wa somo hili tumeutaja ubaya mwingi tu na tumeujua EPUKA.
§ Kujiepusha na marafiki
wabaya iwe waaminio/wasioamini-2Kor 6:14-18.
§ Kujiepusha na
mazungumzo–Mith 18:7;1Tim 5:20;1Kor 15:33;Kol2:20-21.
§ Kujiepusha na Elimu na
Hekima ya Ulimwengu huu ambayo ni upuuzi kwa Mungu-Efeso 4:13-14; Rumi 16:19
2Tim 2:11-22; 2Kor 10:5; Yakobo 3:17.
Elimu ya jumla ni nyingi
moja wapo ni huwezi kuokoka duniani. Elimu ya Kristo inasema wazi watakatifu
walipo Duniani ndio waliobora-Zab 16:3.
Elimu iliyotawala
ulimwengu huu inayogusa vijana na baadhi wa Kanisani wameipokea na kuiamini, maana
yake hawaamini nguvu ya msalaba ni:-
Huwezi
kuishi KIJANA mwenye afya bila kufanya mapenzi kabla ya ndoa!!
Huwezi kuoa
au kuolewa BIKRA kwa karne hii ‘Mary type’ hakuna leo!!!
Vijana wamepokea Elimu ya Kwanza ikazalisha Elimu ya Pili,
ona juu.
-Shetani anajua wakipokea tu Elimu hizi na kuziamini zitawakatilia mbali. -Watakata
tamaa ya kujitunza kwamba sawa na bure, na wengi wamenasa. -Kumpata Bikra
mwenzio huwezi, bora na wewe jichanganye; wamenasa. -Kufika hadi Ndoa ukiwa BIKRA haiwezekan
ananesha vichocheo, ananasa. Kwa nini ung’ang’ane na Elimu ya Dunia na kuamini
na wewe si wa dunia?
Elimu ya Kristo
iliyosema yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yote yanawezekana mbona hiyo huiamini
na kuitumia ili ukaishi.
Elimu ya Kristo
iliyosema mwili si kwa zinaa pia siijui-1Kor 6:13.
Nikijawa na Neno la
Mungu [Elimu ya Kristo] nitashinda-Zab 119:10.
v) Nijue kuwa niliumbwa
Kutenda Mema nisijifariji kuutii mwili/elimu-Efes 2:10
Kwa vile niliumbiwa
utakatifu Biblia inanitarajia nijizuie -1Kor 9:25.
vi) Mtazamo wa Mungu kwangu
Kijana ni tofauti kabisa na ninavyodhani.
-Rika ya
ujana natarajiwa kumkumbuka/kumuabudu Mungu-Mhu 12:1.
-Nizo
nguvu si za ugali na maharage bali za kumshinda muovu-1Yoh 2:13-14.
Kwanini Mbingu zinaona kijana nina nguvu na
nimemshinda muovu?
-Ninauwezo
wa Kufunga siku nyingi, kuomba kwa muda mrefu bila kuchoka,
-Kusoma/kujifunza
na kutafakari Neno la Mungu na kuliweka moyoni,
-Kutumika
kwa nguvu zangu zote hata sina muda wa kupoteza ila kukomboa.
-Nguvu
za Kiroho zinapatikana katika hayo hapo juu, adui atakupataje?
Nguvu za Kiroho zinakusaidia kuushinda
mwili, changamoto, dunia n.k.
Nguvu za Kiroho zinakuweka karibu na
Mungu na adui lazima akukimbie
Nguvu za Kiroho zinakupa ufahamu wa
kumjua Mungu na Neno lake.
Nguvu
za Kiroho zinanipa uwezo wa kumuamini Mungu si wanadamu.
Nguvu
katika Roho Mtakatifu na kuwa chini ya uongozi wa Mungu.
-Nawaandikia ninyi vijana kwasababu mnazo nguvu, hata nguvu za
kimwili tulizopewa pamoja na kutusaidia kiuchumi, elimu pia zipo kutusaidia
kupata nguvu za Kiroho. Kijna usile mwaka mzima funga, omba kwa afya
Kiroho/mwil.
Tangu siku za Yohana
Mbatizaj Ufalme wa Mungu unapatikana…..-Math 11:12.
Ili upate vitu vya
Ufalme wa Mungu lazima uwe na Nguvu si kilegelege hivyo.
Ili kuteka kitu lazima umfunge
mwenye nguvu, na ufalme ni hivyo kama mwili unanguvu utiishwe, hekima za dunia zitiishwe
ili uteke vya ufalme-Math 12:29.
Ili uje upate mke/mume
mwema aliyejaa nguvu hizo lazima uwe na nguvu.
Ili upate Baraka za
Ki-Mungu hata kwa maisha ya kimwili lazima uwe na nguvu.
Kwahivyo, unahitaji
nguvu ili kuutunza Ujana wako si kwa ulegelege. Nikizembea katika kutafuta
nguvu nikajikuta nimezini yapo MADHARA yake.
3.
NIJUE BAADHI YA MADHARA
[20] YA KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA
i) Kumtenda Mungu dhambi [Yusufu]–Mwanzo
39:6-9; Rumi 8:6-8; 1Kor 6:15-20.
ii) Kuharibu ushuhuda
[Wokovu unatukanwa] – [aibu] Mithali 6: 32 – 33.
iii) Kufungua Mlango wa
mapepo/kupokea maroho ya unayezini nae – 1Kor 6:16.
iv) Kuishi na Hatia Moyoni
hasa dhambi isipotubiwa – [fedheha] Mithali 6:32-33.
v) Kuishi na Majuto
maishani maana kumbukumbu haifutiki – 1Kor 6:18 – 20. Dhambi hii inafanyika juu
ya mwili wako ndio maana haifutiki. Toba ya Kweli Mungu atasamehe na
kusahau-Ebrania 8:12, lakini wewe hutosahau kamwe.
vi) Kujichukia na Kumchukia sana
mtu uliyeanguka naye, misisimko yote itaisha-2Samweli 13:1-22. Kuna kisa cha
kusikitisha cha Kijana Amnoni na Tamari.
vii) Kuwa hatarini kuingia
katika anguko tena-kwa mwili kudai haki yake kwa
Kasi maana
umechokozwa. Utaingiwa na roho ya
kutoshiba-Ezekiel 16:28-30a.
viii) Kuua nguvu ya kujizuia,
kuudhibiti na kuuweza mwili- 1Kor 6:13; 9:25. Ndipo mambo ya kuchua/kupiga
punyeto [masterbation] yanapoingia Kanisani, malkia na wafalme bandia
wanaponunuliwa na vijana kwa matumizi machafu. Kuchua, kutumia malkia/wafalme
bandia ni ukahaba tosha-Ezekiel 16:15-17.
ix) Kuwaumiza wazazi wako na
Kanisa la Mungu wewe ni kiungo – 1Kor 12:12-26. Tunaudhaifu katika mapambano
maana kiungo wewe umejeruhiwa na nafasi yako inaupungufu, pia tunaposimama kama
Kanisa unatutia doa/dosari.
x) Kutoaminika kwa
Mungu,Wazazi,Kanisa na Kutojiamini-Maombolezo 1:8a.
xi) Kupata Mimba/Watoto
wasiotarajiwa; wote kaka/dada mnapata mimba/watot. Ni aibu sana ukiwa Kanisani kupata/kutia
mimba/watoto wasiotarajiwa.
xii) Kupata magonjwa ya Zinaa
Kaswende, Kisonono, Gonoria, Ukimwi n.k.
Ni aibu kijana wa Kanisani kupata magonjwa ya zinaa akiwa Kanisani.
xiii) Kuua ndoto zako. Ukishapata
mimba/mtoto/ukimwi ndoto zinaishia hapo.
Ndoto ya wengi ni kuoa au kuolewa akiwa bikra, asilale na mtu kabla
ya ndoa.
Utaiua
ndoto hii nzuri ya Ki-Mungu inayotaka kila mtu awe na mke/mume wake mwenyewe
1Wakor 7:2; Ilikusudiwa hivyo tangu awali-Efeso 2:10.
xiv) Kulipa gharama kubwa ya
kurudi katika nafasi yako kiroho na kimwili pia.
Kihuduma
kurudisha viwango ni gharama kubwa, masomo kuanza tena ni gharama kubwa, kwa
wazazi/jamii kukupokea kama mwanzo ni ngumu. Na BIKRA hiyo ndio utalipa gharama
ya kukubali matokeo maana hairudi si kwa kijana wa kiume au wa kike
uki-unsealed hakuna muujiza wa ‘resealed’.
xv)Kuchakaza maumbile yako wavulana/wasichana–Wimbo Bora 8:8,9,10.
Malkia-uke unaukuta[bikra] kwa kulala na mvulana tu ukuta
unaondoka-8:8.
Ukuta ukitunzwa hadi
ndoa ni heshima na furaha kwa Wazazi na Kanisa-8:9.
Ukuta ukitunzwa hadi
ndoa ni heshima na kibali cha ziada kwa ‘mr’ wako-8:10.
Inatisha sana ukuta
kuondoshwa binti akiwa ameokoka na yupo Kanisani. Dada ambaye umeokoka huna UKUTA utunze UKUTA
wa Roho Mtakatifu sasa. Na endapo utaolewa ukiwa umejitunza kwa jinsi hii kwa
maumbile ya uke ‘mr’ wako atajua umejitunza hata kama UKUTA haupo. Miaka yako katika WOKOVU ifanane na hali
halisi ya Malkia wako. Sio Miaka 5 ya
Wokovu lakini Malkia anaonesha ni Muongofu Mpya wa miezi 5 tu ya baada ya kuchumbiwa-AIBU!
Mfalme-uume unaharibiwa na wanawake/kupata jeraha-Mith 31:3; 6:32-33.
Kibinaadamu wakaka wanadhani wako salama kwa vile hawana alama ya wazi. Ki-Mungu Biblia inaonesha wazi kuwa wafalme wanaharibiwa na wanawake na kuna jeraha lisilofutika na kuvunjiwa heshima kwa kaka aliyezini. Kaka anatoka akili kila anavyozini na alama Mungu aliyoiweka kwa mfalme used haifutiki. Mungu anatutaka wote wakaka na wadada tuwe BIKRA na INAWEZEKANA. Maswali ya wewe mzima yaulizwe kote kote si kwa dada tu. Biblia imetoa ‘Gender Balance’ juu ya hili na kuonesha madhara na matokeo ya kaka kuzini >Kutoka akili – aziniye na mwanamke hana akili kabisa, anaingamiza nafsi. >Jeraha na fedheha haitofutika – Mithali 6:32-33; 20 – 26; 7:1-15; 21-23. >Haifutiki moyoni maana hufanyika juu ya mwili wako wote – 1 Kor 6:18 – 20. >Ni kweli kuwa kwa toba ya kweli Mungu atasamehe/atasahau-Ebrania 8:12. >Wewe hutosahau kamwe tendo hilo hata kama ni dk 5 tu, maana linahusisha >>Moyo wako wote, Akili zako zote, Nguvu zako zote na Mwili wako wote. Na Inasikitisha kijana kuanza ngono akiwa tayari ameokoka na yupo Kanisani.
Kibinaadamu wakaka wanadhani wako salama kwa vile hawana alama ya wazi. Ki-Mungu Biblia inaonesha wazi kuwa wafalme wanaharibiwa na wanawake na kuna jeraha lisilofutika na kuvunjiwa heshima kwa kaka aliyezini. Kaka anatoka akili kila anavyozini na alama Mungu aliyoiweka kwa mfalme used haifutiki. Mungu anatutaka wote wakaka na wadada tuwe BIKRA na INAWEZEKANA. Maswali ya wewe mzima yaulizwe kote kote si kwa dada tu. Biblia imetoa ‘Gender Balance’ juu ya hili na kuonesha madhara na matokeo ya kaka kuzini >Kutoka akili – aziniye na mwanamke hana akili kabisa, anaingamiza nafsi. >Jeraha na fedheha haitofutika – Mithali 6:32-33; 20 – 26; 7:1-15; 21-23. >Haifutiki moyoni maana hufanyika juu ya mwili wako wote – 1 Kor 6:18 – 20. >Ni kweli kuwa kwa toba ya kweli Mungu atasamehe/atasahau-Ebrania 8:12. >Wewe hutosahau kamwe tendo hilo hata kama ni dk 5 tu, maana linahusisha >>Moyo wako wote, Akili zako zote, Nguvu zako zote na Mwili wako wote. Na Inasikitisha kijana kuanza ngono akiwa tayari ameokoka na yupo Kanisani.
Nakupa pole unayejifariji kufanya dhambi hii ukidhani hawapo tena MABIKRA.
Dhana hiyo haikuanza leo tangu waandishi wa makala hii tukiwa ‘single’ dhana ilivuma
hawapo mabikra kumbe tupo na tukaoana tukiwa BIKRA kaka na dada. Na tumekutana
na wanandoa wengi waliooana wakiwa BIKRA kaka na dada. Mabikra hawatakoma
katika nchi maana katika kila jambo la Ki-Mungu masalia wataendelea kuwepo hata
uovu uzidi sana. Kaka kuwa wa Kwanza kwa DADA na Dada kuwa wa Kwanza kwa kaka
SIKU YA NDOA ni Jambo la Ki-Mungu. Ni
Muhimu kuishi maisha ya uaminifu kamwe
usijifariji kwa dhana hiyo potofu.
Ni wote tunapaswa kujilinda na kujitunza hadi NDOA – Mithali 5:1-5;
9:13-16. Sio Malkia watunzwe, Wafalme waharibiwe hakuna fundisho hilo katika
Biblia. Dhambi ni dhambi kwa wote, misisimko ya mwili ni wote, uzembe wa kuutii
mwili badala ya kuutiisha mnafanya wote, kwanini BIKRA awe dada tu? Tunatamani tunapomaliza kipengele hiki cha
kuchakaza maumbile ufunguke. Usiulize maswali ya upuuzi kwa mchumba wako, “Vipi
dada wewe ni mzima” nawewe je, kaka ni mzima? Au unataka kuvuna usipopanda?
Hakuna Kanuni hiyo kwenye Biblia-Wagalatia
6:7; Wakolosai 3:25. Umeondosha kuta za wasichana tele tena mpaka upo
Kanisani, inafika kuoa unataka mzima atoke wapi? Kuna wenzio kuliko wewe
ulipoondosha kuta 5 wao wameondosha 15.
Ukipata mchumba/mke mzima ni neema tu usiifanye ni Kanuni ya kusimamia. Ikiwa umeomba na umempenda kwa dhati maswali
yanatoka wapi? Upendo hustiri wingi dhambi 1Pet 4:8,Upendo una adabu-1Kor 13:5.Upendo
wako vipi?
Mkazo huu ukuguse moyoni kaka/dada bikra muendelee kujitunza, uthamani
wa Ubikra wako ni mtaji mkubwa kwa hatima yako ni zaidi ya fedha/dhahabu. Mungu
amekuokoa, amekuwahi USIICHEZEE NEEMA
HIYO wengi wanaililia, jiombee sana huku ukizingatia yale mambo ya mwanzo
wa somo ili kujilinda.
xvi)
Kaka
kupoteza mbegu za uzazi-unatoa wakati sio, kwa mtu siye, mahali sio.
Dada naye anapokea mbegu za uzazi-wakati sio, kwa mtu siye,
mahali sio.
Wakati muafaka ni Ndoa, mtu sahihi ni Mwenzi wako, uchochoro
huo sio.
xvii)
Kaka/Dada
wote kupoteza nguvu kwa kutumia kwa ngono hiyo-Mith 31:31
Nguvu ambayo ingetumika kwenda kushuhudia inatumika katika
ngono.
xviii) Dhambi hii ikilelewa na
kijana mwisho hupelekea kutamani wake/waume
za watu. Kawaida ya uovu
unakua, hukuweza kumuogopa Mungu na ukafanya ngono na wanafunzi wenzio
Sekondari au vijana wenzio wadogo Kanisani mwisho unaona wake/waume za watu
wote sawa tu na hao. Kijana unaanza
kumendea wake/waume za watu kwa kutotunza ujana wak.
Biblia imeonya vikali
hapa, usidhani uko salama ni hatari-Mith 6:27-29. Inaonesha kuwa makali ya moto
yatakuwa kifuani mwako, hauko salama. Wengin sawa na baba/mama yako unapata laana
kuona utupu-Walawi 18:7
Vijana wengine huona ni
bahati kuwa na mke/mume wa mtu hiyo ni balaa, nuksi, mkosi huo, kwanini uone
sawa ku-share na mtu? Walawi 18:16;20.
xix)
Madhara
ya Dhambi hii kwa Kijana hata akiingia katika Ndoa ni:
>Dada atapata aibu
kwani mumewe atajua kuwa hakutulia Kanisani alitulia siku chache karibu na
kuolewa na pengine akawa na mimba isiyo ya ‘mr’.
>Dada kutoaminiwa na
mumewe na kuishi kwa mashaka katika Ndoa.
>Kaka naye ikibainika
hakutulia Kanisani mkewe hatomuamini ni hatari.
>Mume/Mke kuua nguvu
ya mguso wa upendo wa mvuto kwa T. Ndoa.
>>Kwa kuwa amezoea ku-sex na malkia/wafalme wengine
Kanisani/nje.
xx) Kufungua Mlango wa Adui kukuhubiri nani zaidi kati ya mafataki na ndoa.
Kuvutwa kumbukumbu ya
‘sex’ ya kabla ya Ndoa kupambanishwa na ndani ya Ndoa. Ni rahisi sana kugundua nani zaidi kwa vile
Tendo ni lile lile ila tofauti ni kabla ya Ndoa ni HARAMU na Ndani ya Ndoa ni
HALALI. Sasa ukizoea dhambi hii Kanisani tena kwa siri, hakuna toba ya kweli, haujatengwa
iabishwe, haijulikani kwetu ila mwili wako unajua ni HATARI.
Unaweza kuoa/kuolewa na
mume mzuri/mke mzuri tu lakini tatizo likawa hakidhi uhitaji wa kimapenzi kwa
namna ya mwili wako ulivyouzoesha kabla ya kuoa/kuolewa hili tayari ni tatizo
kubwa linalotikisa NDOA.
Tunapomalizia madhara
hayo ishirini [20] kati ya mengi ya kufanya mapenzi kabla ya Ndoa; tunakusihi
wewe ambaye hujaguswa na hujagusa Usijaribu na mwenye Ukuta wa Roho Mtakatifu Usitende dhambi tena. Wote
tuipate THAWABU ya wanaovumilia hadi mwisho-Mathayo 24:13.
4.
HITIMISHO
i) Ishi ukijua kuwa umekufa
kwa dhambi unaishi kwa roho-Warumi 8:5-10;
Na ukiishi kwa roho
hautazitimiza kamwe tamaa za mwili/ujanani-Gala 5:16.
ii) Ishi kwa tahadhari sana
huku ukijiangalia usianguke – 1Kor 10:12-13.
iii) Usijiamini kupita kiasi
[over confidence] kwa kigezo cha andiko Rumi 6:2-11.
Kuna watu wamejiamini
kupita kiasi kwa andiko hili, busu maiti mara inafufuka.
iv) Ishi kama mtumwa wa
Mungu uko huru lakini huko huru- 1Pet 2:16; Rum 6:12-14.
Kijana wewe ni mtumwa wa
Mungu na Yesu ni Bwana wako mipaka ni lazima.
Mipaka katika Mavazi,
Marafiki, Mazungumzo, matendo, mahusiano, masaidiano, muda, mikutano[mahali pa
kuwepo], mawasiliano kwa ujumla, Mipaka
kwa mwenendo mzima hasa kwa jinsia 2 hizi tofauti-ni hatari kugandana
kama ruba, ni hatari kufatana kama kumbikumbi, ni hatari kuambatana gizani sisi
ni wa nuruni. Mungu akupe neema ya kushinda mwili unaokuvuta huko na uweke
mipaka kila eneo kwa damu ya Yesu na kuhakikisha huvuki wigo huo ili UTUNZE
UJANA WAKO na Utumishi wako usilaumiwe kwa kusababisha mwenyewe tuhuma hizo. Vyanzo vya Vijana wengi kulaumiwa hata kama
hatujafanya jambo ni KUKOSA MIPAKA.
Kuutumia vibaya uhuru wetu na undugu wetu katika Kristo ila wewe usiwe
hao.
v) Ishi kwa kufuata hekima
ya Mungu si wanadamu – Yakobo 3:17; Rumi 16:19b.
vi) Subiri wakati wa Bwana
[Ndoa] – Mith 6:20; 26; 7:1-5; 21:27; Mhubiri 3:1. Usijidhalilishe kwa mtu
asiye wako, mara Mfalme ‘anamatege’ au
‘anamaganda’ yatanadiwa mji mzima. Malkia
‘anamakovu’ anayaona fataki. Mtu aliyewako hata akute mapungufu atakupokea
jinsi ulivyo maana amepewa na Bwana. Subiri Ndoa.
vii)
Jizoeshe
kuliishi Neno la Mungu ili uwe na adabu neno huadibisha- 2Tim 3:16.
Biblia inasema wazi neno hutuadibisha, hututia
adabu ya kuongea, kutenda n.k.
viii)
Inawezekana
kabisa kutunza ujana wako hadi ndoa–Marko 10:27;Matha 19:26.
Yasioyowezekana
kwa wanadamu kwa Mungu yote yanawezekana, AMEN.
**MWISHO**
Njema sanaaaaaaaaaaaaaa my dia, i have learnt alot although mengine itabidi nikuone koz cjaelewa kabisaaaaaa
ReplyDelete