SINGLE LADIES are you online??
Niliandaa mawili matatu kwa ajili yenu kila nikitaka kuyapublish najisahau.Wiki hii tutaongea kwa picha na maneno kidogo. .
Kila Binti anapofika umri fulani huanza kupata shinikizo toka kwa jamii,familia kuhusu KUOLEWA.Wakati mwingine hata yeye binafsi huanza kujihoji mbona kama umri wangu unakimbia na hakuna mwanaume yeyote anayenitamkia ndoa.
Leo nataka nikutie moyo SUBIRI WAKATI WA MUNGU!
●Ndoa si mashindano ya riadha.
●Ndoa si kitu cha mkumbo
●Ndoa si kitu cha kutambishiana
Usifanye makosa kama haya ya Mwanzo 19:31-32 hawa ni mabinti kama mimi na wewe ambao waliamua kutafuta shortcut kwa kuamua kuzaa na baba yao baada ya kukosa waume wa kuwaoa..
Wewe si wakwanza kuwa single mpaka muda huo ulio nao.Kaa miguuni pa Mungu ukisubiri,jilinde dhidi ya njia mteremko zozote ambazo pengine mabinti wenzio wanafanya kama kupata ujauzito kabla,kuhamia kwa mwanaume kabla hata ya kuchumbiwa nk.
Ndoa ni jambo la milele,ni jambo la kudumu hivyo chaguo na maamuzi yeyote utakayofanya yakiwa mabaya/yakukurupuka/ya mkumbo ni WEWE BINAFSI utakayekabiliana nayo.Si marafiki,wazazi au ndugu watakaokusaidia.
KUSUBIRI WAKATI WA MUNGU
Kama kuna jambo huleta maumivu na taabu ni kile unachokitamani au kukisubiri kwa shauku kikichelewa.Sasa kuna yale tunayotamani na kuna ambayo Mungu anaona tunastahili kuwa nayo na ndiyo aliyotuandalia na kutukusudia.
Kusubiri sio jambo rahisi na si wote wanaoweza.Mara nyingi kama mtu ni dhaifu anaweza kuchukua shortcut kama nilizosema hapo juu.
Nikuombe binti mwenzangu usubiri..Mungu analijua hitaji lako toka kuumbwa misingi ya dunia.na yupo mume wako anayekusubiri pia ni vile wakati haujafika.
Unaweza kuwa unapitia upweke na mahitaji ya kibaiolojia lakini Mungu anaweza kukusimamia na kukushindia mpaka mwisho.
Maneno na kashfa za walimwengu yawezekana zinakulemea nakuombea usipanic..usifanye maamuzi ya pupa yatakayokufanya ujute au uishi kwa huzuni kuu.
Mungu anakufahamu na analijua hitaji lako kwa wakati atatenda.
Acha kujilinganisha na wengine..hujawahi sikia mtu yupo kwenye ndoa lakini hana amani..furaha nk sasa kila mtu ana pito lake.
Olewa kwa sababu wakati wako umefika na si kwa shinikizo la awaye yule..
Mungu awe nawe mrembo..mumeo yupo tu endelea kuyafurahia maisha yako, Usijirahisishe,usifuate mkumbo nk.
Loved you're!!Tchao
No comments:
Post a Comment