Sweethearts ninakuja na kitu kipya hapa special kwa sisi tu maana kuna vitu vingi na vya muhimu ambavyo wengine hampati fursa ya kujifunza nyumbani au kutokana na sababu fulani hukuyafahamu au kama unajua tutakumbushana si ndio enheeee kama nawaona vile warembo wangu mnajiandaa kupata vitu...Yees tuombeane uzima japo blogger na mie nina shule imebanaa hapa nitaweka ratiba vizuri ili twende sawa ili nisikose mwana na maji ya moto...
√tutapeana dondoo za usafi na jikoni kidogo..
√tutapeana dondoo za kufanikiwa katika ile mpango tuliyonayo.
√tutapeana mafundisho ya namna sisi kama wanawake tulivyo na uhusiano wetu na Mungu maana tuna nguvu nyingi ambazo hatujajitambua.
√Afya yetu as ladies...
THIS WEEKend duty
°kama uko nyumbani jitahidi uwezavyo kusaidia kazi...amka mapema jishughulishe hata kama kuna dada wa kazi shirikiana nae sio umeamka mipango lundoooo ooh nywele zangu,oooh kucha zangu no if we expect being great wives lazima tufanye kazi...at times utaona kama unaonewa wee lakini jua fika lazima ukiwa na kwako utafanya kazi....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment