HAPPY WOMEN'S DAY..to us all women in this planet..
Mwaka huu ni mwema kwetu..nilifurahi binafsi kujua maadhimisho haya yameangukia jumapili..Ilinipa flavour ya kitofauti maana mwaka jana nilizungumzia kijamii zaidi..
Najua wajua vile mambo yanakuwa ukimhusisha Mungu kila jambo la maisha yako..Hata unapomuambia yale ya ndani huyafanya..
Stop crying girl,ni wakati wako wakurejesha thamani yako na kufurahia maisha yako.
Mwaka huu si haba tukamegeana vipande vya baadhi ya masomo ya Joyce Meyer wengi twamjua..ukihitaji zaidi pekua moja ya makala zangu nilimwandika kama mwanamama wa mfano kwetu hasa wenye ndoto za kufika mbali na ambao pengine mlikumbana na every hard PAST she is truly a strong and inspirational..
☆☆☆★★Leo tuanze sasa na hili la "KUJIAMINI KATIKA THAMANI YAKO"
●Chukua dakika kadhaa,utazame moyo wako..
☆unajisikiaje kukuhusu?
*kama jibu halikuridhishi au halikubaliani na vile Mungu anakutazama..Nakutia moyo kuanza kutafuta mwangaza wa namna Mungu anavyokutazama..
*Jitazame kama Mungu anavyokutazama kuwa wewe u mtu wa thamani..gharama..anayestahili kufika mbali kwenye zile ndoto alizonazo..Kupitia neno lake amesema hivyo na anasisitiza kabla ya kutungwa kwa mimba zetu alitujua na kutuchagua..
Inawezekana wazazi wako walikwambia ulizaliwa kwa bahati mbaya(accidental child)hilo si tatizo HAWAKUKUHITAJI WAO ila MUNGU alikuhitaji mno mnoo.
♡♡Simama ukiwa na ukiri sahihi juu yako..wewe ni wa thamani na mwenye kesho njema ..Mtu yeyote asikushushe..
ISAYA 43:4-5
Source:The Confident Woman Devotional(2011)By Joyce Meyer.
No comments:
Post a Comment