Kwa nini unatazama nyuma tena?
Kipi tena hicho ulichosahau?
Si wewe uliyetamani kesho ije..ni vipi tena waikumbuka jana?
Si hiyo JANA iliyokupa maumivu na kukupotezea muda?
WHY..KWANINI?
Leo nizungumze na wewe uliyeamua kusonga mbele na maisha yako hasa kutokana na uliyowahi kuyapitia kwenye maisha si rahisi kujua ni changamoto gani lakini wewe binafsi unajua..
Baada ya hilo ukaapa kuwa jambo hilo limekufunza umekomaa haswa na hutolirudia..pia umeamua kuendelea mbele na maisha yako.Ulishaanza kupiga hatua
Sasa nini leo tena unataka kuyabadili maamuzi yako ambayo pengine yamebeba ushindi na funguo ya maisha yako yaliyojaa furaha na baraka tele huko mbele.
Mara nyingi hofu na kutokujiamini kuwa ulichokiamua ni sahihi hupelekea kugeuka nyuma..
Jiamini tu ulichokiamua ni sahihi..usonge mbele..
Kuna milango lazima uifunge tu wewe binafsi na kutotamani kuifungua tena kwa ukuaji wako binafsi na mafanikio katika yale uliyojipangia
No comments:
Post a Comment