Natumaini sote tuko sawa..tutaendelea na mfululizo wa masomo ya Joyce Meyer kutoka kwenye kitabu chake cha Confident woman devotional..
DAY 2 alizungumzia kuhusu WOGA/HOFU..Japo kitabu chake ni dira nitakua naongezea pia vitu kidunchu..
Kama kuna jambo linatuchelewesha kufika tunapotaka..kufanya tuliyojipangia au kufanya maamuzi sahihi ni vitu hivi pacha.
Ni Woga/hofu..
Ya kuwa itakuwaje nikifanya jambo hili likashindikana.
Au vipi nikiamua maamuzi haya nitaelewekaje au kuonekanaje?
Joyce alianza kwa kusema"Japo wapo watu mashuhuri wanaochukua hatua kufanya mambo makubwa ya kuduwaza haina maana HAWAOGOPI"
Mfano:-1*Katika agano la kale hata shujaa ESTA alijisikia hofu alipoombwa kuingia kwa mfalme na kuiacha familia yake na maisha aliyozoea..
2*Hata Joshua alipoachiwa mikoba ya Musa juu ya kuwafikisha wana waIsrael nchi ya ahadi(kaanani)aliogopa pia..
3*Joyce Meyer binafsi anakiri kuogopa sana alipoambiwa na Mungu kuacha kazi na kuja kumtumikia..Anasema siku ya kwanza kuhubiri aliingiwa na hofu saana magoti yaliishiwa nguvu alitetemeka mno,alilegea sana na alijua angeanguka..
HOFU HAIMAANISHI U MUOGA/MJINGA..=humaanisha kuwa ●●●Unapaswa kuwa radhi na tayari kuingiwa hofu bila kuvurugwa nayo kuyafanya yale UNAYOPASWA AU KUAZIMIA KUFANYA..
■>>Hofu ipo na itaendelea kuwepo mradi tu wewe binafsi kutoipa kipaumbele cha kuwa uzio au ukuta kutimiza zile ndoto na mipango yako..
EZRA 3:3-4
Kwako mwanamke mwenzangu au mpenzi wa ukurasa huu pengine bado unaogopa kufanya baadhi ya mambo au hata maamuzi..
Hebu jiamini na umuombe Mungu akupe ujasiri uyafanye yote uliyoazimia.
Ukiruhusu hofu tu na woga itakuwa ngumu hao watu unaowatazama na kuwaadmire walithubutu na si kwamba hawaogopi..la hasha ni vile tu wameamua kutoupa woga/Hofu nafasi..
2015 ni mwaka wa kibali na utofauti sasa usijichimbie kwenye woga jitokeze..jiongeze kuelekea kwenye mafanikio..
MUCH LOVE♡♡♡♡♡
Source:-Joyce Meyer"Confident woman devotional"(2011)
Plus my own additions..
No comments:
Post a Comment