Hello cute ladies!! nina tumaini tuko sawa,tunasonga mbele..
Kuna jambo leo nataka tutete kidogo..
Nilipata hili lalamiko muda kidogo nikasema nijipe muda nilipembue, nilipitishe kwa wenye umri zaidi ya wangu,nisome makala za watu kadhaa nikiiva niliongezee busara zangu nilijibu huku ili sote tujifunze kama mwenye swali alivyopenda..
Dada mwenzetu aliomba ushauri kuwa yupo kwenye uhusiano na kijana ambaye ni mgumu mnoo kumhudumia hata kwa kitu kidogo mpaka akawa anajisemea kuwa wallet yake imefungwa kwa soleksi..Hebu leo tupeane mwanga hapaUnafanyaje ikiwa ni wewe..
√ Unapoanzisha uhusiano na mtu ni vizuri kuwa flexible kutokwenda na matarajio lukuki kwamba kila unalotaka litatendeka na kuwa jinsi unavyotaka.Jiweke katika hali ya kutovunjika moyo au kukimbia kwa utakayokumbana nayo huko.
√Ni vizuri pia kujua au kumfahamu mwanaume uliye naye ni wa aina gani?(background), mwingine alilelewa kwenye familia za kijungujiko..kwa kujinyima sana kwa hiyo kila alichonacho anaona akimpa mwingine ye atabaki na nini?au mwingine uchoyo ni tabia yake..When you know better you do Better
√Ni vizuri pia kutokujilinganisha na mashosti au mtu awaye yeyote..Mfn rafiki zako woteee hupelekwa maeneo ya gharama kula starehe,shopping za gharama nk.ni vizuri kuridhika na pale ulipo maana tamaa ya mali yaweza kukutoa kwenye upendo wa dhati na kukutupa kwenye taabu ya milele..kuna msanii akaimba bora kucheka kwenye bodaboda kuliko kulia kwenye range Rover..
√Mushirikishe Mungu mweleze kwa dhati nna unavyoumia na tabia hiyo ya mwenzi wako..kwake hakuna linaloshindikana kama aliubadili moyo wa farao,akabadili tabia ya sauli aliyeshindikana atakusaidia tu.
√Jitume..tafuta vishughuli vitakavyotuliza baadhi ya mahitaji yako kama binti huku bado ukimheshimu na kumpenda maana hakuna mkamilifu..Yawezekana ni mwema kwa mengine ila tu mkono wake ni mzito katika kutoa na kukuhudumia..
Love u sweethearts!! tujitume..tumtegemee Mungu anayo majibu ya mahitaji yetu yooote..Kabla ya kulia na kuchanganyikiwa kwa uhusiano ulio nao PIGA GOTI..muombe Mungu be strong &stay beautiful
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment