kusahau tumeumbiwa binadamu..Hii kauli naisikia mara nyingi mnooo hasa linapotokea jambo lililotaka uwajibikaji ila mhusika akajisahau au kufanya tofauti na alivokusudia..
Rafiki 2014 hiyooo inakaribia kwisha nadhani yapo uliyokumbana nayo yakukufurahisha na kukuumiza hadi umeapa au kuandika kwenye diary sirudii tena mambo/maamuzi haya.
√Kama hukuwa mtu mwenye kutunza misimamo na maamuzi yako..Jitahidi mwaka ujao kujipanga ili kuzuia hasara na maumivu ya kujitakia.
Iwe kiuchumi,kimaisha na angle yoyote ile.
Ni imani yangu mwaka ujao tukijaaliwa kuufikia utakuwa wa tofauti nawewe ukifanya majumuisho yatajaa kujipongeza na si kuumia na kujilaumu.
Usiwe mwaka wa kusema ningejua...ningejua but it become too late..Tuangalie mifano hii-**_
**wa mlevi anaependa kupata kilevi atakunywaaa..atalewa..mwingine atarudishwa mpaka nyumbani kwenye toroli ila kesho anarudi tena..
*****Au wakati mwingine una pesa ulizopata kwa shidaaa na kujinyima mnoo.una plan vizuri ila likitokea la kuzifuja unasahau namna ulivyozitaabikia..
******Mara nyingine tujifunze hata kwenye maumivu unayokutana nayo kwenye love life yako..leo umeumia kesho unarudia jambo lile like lililokugharimu..
Jifunze kutokana na makosa na uyatendee kazi ulojifunza huku ukimshirikisha na Mungu maana kuna maamuzi hayawezekani mpaka amehusishwa..la sivyo unajikuta unajisahau na kurudia jambo lile lile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment