Heri ya Pasaka wapendwa wangu!!!Naamini KRISTO amefufuka mioyoni mwetu na atafufua na yale yaliyokufa kwenye maisha yetu...!
Sikukuu hii ilinijia vyema sana.Nilikua naburudika na wimbo wa Angel Benard ITS A NEW DAY..!mara ya kwanza ilikuwa ni burudani tu lakini baadaye niliguswa mnoo na maneno yaliyomo ndani...
Mara nyingi kwenye maisha kuna mambo mengi yanatutokea mazuri na mabaya kwavile sote tuko kwenye kalenda ya Mungu hutupasa kuyapokea na huku kibinadamu yakiacha alama ya huzuni ama furaha...
Jana ya maisha imekuwa ikichukua nafasi kubwa mara nyingi hasa kutokana na ubaya au maumivu inayokuacha nayo..Lakini kwenye wimbo huu mtunzi anasema JANA kwaheri....acha uende si kuwa umeniumiza pekee na mafunzo umeniachia.Nitakavyokuwa LEO si kama JANA...
Kama unataka kutokupiga hatua ni kukumbatia mambo yaliyopita yawe ni ya mapenzi,maendeleo uliyoyakosa ,mateso,manyanyaso ,nk!!
Ukitaka kushinda haya,amini Kila jambo lina wakati wake....
√wakati wa kupanda na wa kuvuna
√wakati wa kupata na kukosa
√wakati wa kulia na kucheka..
Samehe yote...Jivike ujasiri songa mbele..
Jana imepita yape macho yako fursa kuona mwangaza mpya...Leo ni kipimo cha ukomavu wetu kwa baadhi ya experience zetu za hapo nyuma..
LET IT GO....!
Future will be so great and lighter if your past burdens are not with you...Mungu pia akusaidie unapochukua hatua kuiacha jana na kuitazama leo yako..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment