Friday, March 21, 2014

weekend notice board!!

 Jumamosi hii tupitie usafi wa chupa ya chai,chupa ya maziwa ya watoto,vifàa vya jikoni kama vya kutunza sukari,chumvi,mafuta,viungo,keto za kuchemshia maji nk..

kwa upande wa chupa ya chai..
>Ifungue..tenganisha vile vifaa vya ndani..huku ukilishikilia lile yai kwa makini.
>andaa maji yako ya uvuguvugu na sabuni bila kusahau osheo..
>tumbukiza vifaa vyote vioshe mpaka ving'ae..
>suuza kwenye maji ya kutosha..
>anika /futa kwa kitambaa safi..
Then rudishia vifaa vyote kama awali...

Hatua hizi zinaweza kutumika kwa vyombo vyote nilivyotaja..ila kwa zile plastic keto usiingize maji yale maeneo unayounganishia na umeme..

Love you all..
weekend njema...

No comments:

Post a Comment