Thursday, March 20, 2014

Wazazi ni wazazi tu wana mchango mkubwa kwako!!

Leo tuangalie eneo la wazazi /walezi tulio nao..
pengine wametangulia mbele za haki lakini wapo 
ambao wanakulea.



Ni kweli tunakua na tunakwenda mazingira mbalimbali..upo shule,kazini au popote umekutana na marafiki au watu wa mhimu sana kwenye maisha yako pengine kutokana na mazuri wanayofanya within a fraction of seconds.. sawa si mbaya lakini wema wao huo hauwezi kufikia walikotoka nawe wazazi/walezi wako...
Najua hata ukifumba macho unawakumbuka vile wamesimama nawe...
kuna nyakati ulishindikana lakini walikupiga bega kwamba wewe ni Kijana wetu haina shida kunasiku 
utakuwa sawa..

Iam so sure unazo kumbukumbu za mazuri yao kwako miaka yote hiyo...so sidhani watabadilika na kuwa waovu now that you're fully grown up..LA HASHA...

Pengine uliteswa na kunyanyasika lakini hiyo haitabadili ukweli kwamba hao ni wazazi/walezi wako..jambo la busara kufanya ni kutambua uwepo wao kwenye maisha yako...KUWASAMEHE na wewe kuwa chachu ya mabadiliko kwenye kizazi kwakuwa kuwa kuna watu ni wabaya si kuwa MUNGU aliwaumba hivyo HAPANA kuna nguvu nyuma yao ukikaa nae vyema huyo mzazi/mlezi utagundua nae aliwahi teswa huko nyuma kwenye safari ya maisha yake au ni hulka tuu...

#hebu kuwa mtu wa baraka kwa wazazi/walezi wako...una chochote kizuri wape...

#uko nyumbani jitume basi wasaidie kazi unapowatembelea au kama bado waishi nao..

#wasikilize wanachoongea hataa kama unaona ni pumba ukilinganisha na kisomo chako utawarekebisha baadaye kwa busara..

#changamoto huwa hazikosi kikubwa ni kumsihi Mungu namna ya kuishi nao kwa busara..
Wazazi na walezi wetu wana mchango mkubwa mnoo kwenye maisha yetu wanaponung'unika juu yetu huwa ni ngumu mtu kufanikiwa..lakini ukiwa na mahusiano nao mema kufanikiwa ni l:alazima  wengine huwaita miungu wa pili...

call them...tell them you love and honour them...

No comments:

Post a Comment