Sunday, March 16, 2014

Bado liko tumaini...

Natumai..una furaha..na matumaini lukuki!!
Kisaikolojia wakati wa kufikiri juu ya kuoa/kuolewa..kina kaka hutamani kumpata mke wa mfano wa mama zao na kina dada hutamani kwa mfano wa baba zao(nitafafanua nikiolewa ha ha ha..tuombeane tu wapenzi wangu wa blogu)

Nikiwa nasoma biblia nikapitia hii verse
MWANZO 25:21"Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake,maana alikuwa tasa.Naye BWANA akamwitikia,na Rebeka mkewe akachukua mimba.."

Mara nyingi kina dada hukata tamaa hasa pale anapokuwa alikuwa kwenye uhusiano ambao uliacha maumivu na majeraha na hata kuona wanaume wote ni makatili na wasio na upendo..nataka nikutie moyo BADO LIKO TUMAINI..wapo kina kaka walio na upendo wa dhati watakaolia na wewe,watakaohakikisha u mwenye furaha na mafanikio..baada ya kuona mstari huo wa Isaka njoo ujifunze kwa watu hawa..

Blogger wenu nikipata fursa napendaga kufuatilia Televisheni baasi nikakumbana na hii couple Giulliana&Bill Rancic
huyu dada ni mtangazaji mahiri wa Tv hasa kuhusu fasheni na Red carpets..Lakini ni survivor wa kansa ya ziwa ambayo imemkosesha fursa ya kupata mtoto kwa kipindi kirefu alihangaika na mumewe ikashindikana mpaka walipotumia njia ya kupandikiza kwa mtu(gestational Carrier)ambapo ilizaa matunda..
Na mumewe Bill ni mjasiriamali,public speaker nk..

nilichokifurahia kwa watu hawa walikua bega kwa bega na hata unapomsikiliza mumewe akiongea naye unauona upendo wa dhati baina ya watu hawa..
Ni wanandoa ambao wapo bega kwa bega kutiana moyo kwenye ndoto na mipango waliyonayo kitu ambacho ni cha faraja sana..
kingine Giuliana anachonifurahisha ni kutoona kwamba kwa sababu nina kansa basi nisijitume NO NO..ni mtangazaji mahiri na anafanya mambo
 ya kijamii mengii..Hivyo na wewe popote ulipo usione shida kufanya mambo yako kwa vile una tatizo fulani labda ugonjwa au lolote unalojua wewe..
Ni maombi yangu MUNGU akupe kufanikiwa katika kila hali..na kuona tumaini au mwangaza pale maisha yako unapodhani yamefika kikomo..
Lots of Love....

No comments:

Post a Comment