Nimekuwa nikipokea maswali na kuombwa ushauri juu ya vingi..ila kuna hiki ambacho kinajirudia..
Mabinti wengi wamekumbana na kudhalilishwa kihisia/kingono(sexual &emotional abuse) na wengine kubakwa au kupoteza ubinti wao kwenye mahusiano yao na vitu hivi vimewaachia maumivu,unyonge na kuwakosesha ujasiri..
Wapo wanaofikiri vingi visivyoweza kumalizika tukiandika hapa..
Ngoja tusome mstari huu AYUBU 22:29
"Hapo watakapokuangusha,
utasema,kuna kuinuka tena;
Naye mnyenyekevu Mungu
atamwokoa"
Ikiwa ulitendewa hivyo,ni kawaida kujisikia uchungu,hasira kisasi na hali yoyote kama kujilaumu nk..Lakini ni vizuri kujua you are not a damaged property.. rape was a crime of violence na tendo hilo lilitokea kinyume na matakwa yako na haukuwa na jinsi kuzuia hilo..
Kuna hatua chache za kufanya..
#1.Tafuta mtu unayemwamini..Uzungumze nae
hisia zako..daima hisia za maumivu hazitoki kwaa kupuuzwa na kuzifukia kwamba hazikuwepo..hapana..Tafuta watu wanaokujali sema kwa ujasiri mpaka usikie uko huru..
#2.Kukutana na taswira za mshituko au hasira unapoona jinsia ya kiume ni kawaida na zisikuumize..wakati utakapojisikia hali hii tafuta mtu atakayekupa hakikisho la usalama na furaha yako..au zikumbuke nyakati za furaha kwenye maisha yako kama binti.
#3.Jitie moyo na uone maisha yako lazima yaendelee..japo matukio hayo yataacha makovu na maumivu jua kuna KUINUKA TENA..
Mungu atakufuta machozi na maumivu yako yote na atakupa mwenzi atakayekuelewa na kuchukuliana na hali yako.
Jisamehe kwanza na uone bado kuna kuendelea mbele...
Mungu bado ni mwaminifu..
Pitia makala za kina Joyce Meyer,Oprah Winfrey&Paula White nao walikumbana na changamoto hizi...lakini leo hii ni wanawake wakubwa na wenye mambo mazuri ya kuigwa.
usijikunyate tena wala kujiona kinyaa..
ur beautiful woman who will have the beat in her life..kisses..

No comments:
Post a Comment