Hellow......
Natumai kila mmoja yuko sawa
.....leo tupitie kidogo suala la kutandika vitanda..unakuta mtu kaamka mapema ila anatimukia shughuli nyingine akija kutandika ni usiku kabla hajalala..
Hapana kitanda kinatandikwa unapoamka na hata hizo shuka na foronya basi zipate maji kwa muda fulani uliojipangia..
Kila mtu hapaswi kuhimizwa juu ya kutandika kitanda... ila leo ninamhimiza binti ambaye baadaye anakuwa mama na mke jitahidi kujifunza na baadaye inakuwa ni tabia yako kutandika kitanda..
Kulingana na godoro ulilo nalo jitahidi kulivisha bed-cover hii itakusaidia godoro lisichafuke na hata unapotandika shuka linanyooka vizuri.
Pia shuka likizidi size ya godoro hutandikika kiurahisi naupendeza sana hata ukilala halichomoki..
Wapo ambao hupiga pasi shuka kabla ya kutandika lakini kama huwezi jitahidi wakati inayaanua baada ya kifua yakunje palepale kambani na ukifika ndani unayahifadhi vizuri.
NB:ni vizuri pia kujifunza kuwa na mashuka ya matumizi ya familia na wageni pia..na kuhakikisha yanakuwa safi muda wote..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment