Katika maisha hakuna formula za maisha zinazofanana kwani kila mtu ana jinsi alivyopangiwa na Mungu kila kitu kiwe..Licha ya hivyo kuna yale ambayo huwa tunayaona yaliwezekana kwa wenzetu tukafikiri na kwetu itakuwa hivyo pia..
Leo tuangalie kuhusu online dating au kwa kiswahili uchumba wa mitandaoni pita kwenye mitandao mingi utakuta mna haka ka collumn (dating site) au wengine wanatumia facebook kujitafutia wapenzi..
Kimekua kitu maarufu sasa kama inaelekea kuwa fasheni lakini ukitafiti utagundua walionufaika nayo ni wachache na walioumia nao ni wengi mnoo...
Online dating si mahala sahihi kwa wewe kumpata mwenzi wa maisha kama kweli uko serious na maisha yako kwani taarifa zinazowekwa na watu si zote huwa sahihi na nina shuhuda za watu waliodhalilishwa kijinsia na hizo skype na mengine na wakaachwa solemba..
Online dating si nzuri kiafya kwani utatumia muda wako wee unaskip meals,unachelewa kulala na hata kuwa addicted na mtandao ili tu kuchochea penzi ambalo uwezekano wa kuleta ndoa ni mchache..
Pia utamaduni wa kiafrika kwenye mambo ya uchumba upoje??
Ninashauri tu huu utandawazi usijekutuacha na majuto na kuona kwamba tulimkosea Mungu kuzaliwa...Hasa watoto wake ndio tunaoumia sana kwa sababu tunapenda kwa kusikia kwa hiyo mwanaume atakupa maneno laini na kukulaghai..tofauti na wanaume ambao kuingia mkenge si rahisi kama sisi
Kwenye celebrities lifestyles hebu tujifunze jambo...sipati shida kwa binti au kijana mwenye elimu na ajira yake ya maana tu akitamani kuwa kama mtu maarufu ulaya..
Lakini sishawishiki leo na binti anayetaka kuvaa kama Beyonce au Kim Khardashian na wengine huku uwezo huo hana..Wenzetu hao walisoma kwanza na kuwa na foundation kutoka kwa familia zao..Mfano Kim alipotoka chuo aliomba mtaji kwa mama yake ambaye alikua anauza mavazi baada ya kufanya kwa miaka kadhaa na dada zake ndio wakakua mpaka leo walipo na lebo yao ya DASH COLLECTION..ni maarufu lakini mwenye msingi..Binti jishughulishe,ridhika na ulichonacho,ila hicho unachotaka jishughulishe kihalali utakipata Iam Here promising you na Mungu anaona haja yako yu radhi kumbariki mwenye juhudi..Utakuwa even more than them...
Stay blessed people........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment