Monday, February 10, 2014
kushindwa si kuhairisha jambo....
Tunayopanga si yote yanafaulu.
Inategemea tu na vile tulivyopokea matokeo kwamba tuliposhindwa ndio basi tena au tutachukua hatua mpya na kusonga mbele.
Tunaposhindwa tunabadili mbinu hatubadili lengo.
Wapo watu mashuhuri ambao mpaka leo dunia inawaheshimu kutokana na vitu wanavyo au walivyofanya lakini haikuwa mteremko kuna wakati walishindwa pia...Lakini haikuwaa mwisho wao walijikung'uta mavumbi na kusonga mbele..
Oprah Winfrey:Hapo alipo sasa ni matokeo ya yeye kukutana nana kukutana na kushindwa kwenye kipindi fulani cha maisha yake..Akiwa ni mfanyakazi wa televisheni fulani aliachishwa kazi kwa ghafla na alipouliza sababu aliambiwa hakuwa na sifa ya kufanya kazi za Tv...lakini leo hii ni mtu mashuhuri sana duniani na anafanya vipindi vya Tv vinavyoyagusa maisha ya watu.
Steve Jobs(RIP):Ameacha alama kwenye upande wa teknolojia ya simi na kwenye upande wa ubunifu..Kampuni ya Apple itamkumbuka saana baba huyu..naye hakuwa na mteremko tu akiwa na miaka 30 alifukuzwa kazi kwenye kampuni aliyoihangaikia sana na alifukuzwa kwa aibu bila hata sherehe au hafla ya shukrani inasemekana kitu hiki kiliathiri maisha yake sana na kumpa msongo wa mawazo..Lakini baba huyu hakukumbatia kushindwa miaka 25 mbele ameacha alama katika ulimwengu huu.
Michael Jordan:Ukizungumzia NBA au mpira wa kikapu unaachaje kumtaja nguli huyu...ametamba dunia nzima kwa mpira kikapu na hata baada ya kustaaafu jina lake liko juu mnoo..Lakini hakuanza tu na kuwa maarufu,akiwa kwenye timu ya shule mwalimu wake aliliondoa jina lake kwenye list..anasema Jordan kitendo kile kilimuumiza mnoo na alipofika nyumbani alijifungia na kulia sana..Lakini hakuvunjika moyo alipambana na leo ulimwengu unamjua kwa umahiri wake kwenye basketball.
Walt Disney:Huyu bwana alikuwa anafanya kazi kwenye gazeti lakini siku ya siku akapokea barua yake ya kufukuzwa kazi kisaa hana ubunifu na maono au mawazo kampuni inayotaka..
hakuishia hapo miaka iliyofata yeye na kaka yake wakafungua kampuni ya Disney ambayo inatupa katuni zote hizi tunazopenda..Haha mie napendaga ya Cinderelaa jamani lol!kwa hiyo ameiachia dunia zawadi japo kampuni yake ilimwona hafai.
Albert Einstein:Baba huyu alikuwa gwiji la Physics ni mjerumani aliyetwa tuzo lukuki..Lakini hakuanzia hapo alipozaliwa mpaka anafika miaka minne kuongea hakuweza ..kwahiyo walinu walipompokea shule wakawaeleza wazazi wake mmh!huyu mtoto kama kuongea tu ni issue je kusoma??lakini Albert alijikita kwenye masomo ya Sayansi na ana quotations nyingi katengeneza zinazotupa moyo na sisi pia.
Natalie au blogger wenu nimekutana na kushindwa pia naupinzani sana
Lakini namshukuru Mungu..Nitashare nanyi kwenye one year annivesary ya hii blogu.
Lengo la kukupa somo hili ni kukupa moyo kwamba kushindwa sio mwisho wa ndoto au mipango uliyonayo endelea kujiamini na kumwamini MUNGU kuwa ipo siku kila kitu kitakaa sawa..
Pengine ni hali ya maisha uliyonayo usikate tamaa..pambana ipo siku utafurahi na kusahau yote..
Kikubwa usichanganye matatizo na kazi au shule..Mfano uko shule unafikiri juu ya umaskini wa nyumbani sasa yale mawazo hayatatui ilo jambo lakini shule hiyo ukiizingatia utapata ajira na kuja kusuluhisha shida mlizonazo..Weka vipaumbele wakati wa kufanya moja lifanye liishe.matatizo yaweke kando.
praying for you...
Winning is our anthem
Unaweza kupata somo hili www.soundcloud.com/BlessedNatalieNkya
au like my Facebook page Blessed Natalie'blog.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment