Monday, February 3, 2014

Kikwamisho haswa kwako ni kipi??Ukikitambua kikabili

Kuelekea mafanikio lazima hasa kujikana na kuwa radhi kuufikia ule mwisho uliouota kwa miaka mingi..Maelezo mengi ya watu waliofanikiwa hayakosi simulizi la jinsi walivyokutana na vikwazo na jinsi walivyojiandaa kuvikabili na kupenya.Kila jambo zuri lina gharama lakini haina maana ikiwa ngumu au kubwa unakimbia la hasha unapaswa kutafuta suluhu.
Baadhi ya vitu vinavyotupa msongo wa mawazo tunapoelekea mafanikio huwa ni :-
√Maneno ya watu haya ni kikwazo namba moja kwani wajuzi wa mambo husema maneno yanauma kuliko kuumwa jino..kuna maneno kutoka kwa watu ambayo usipojua namna nzuri ya kuyakabili hautapiga hatua ng'oo..wapo watakaosema mwee hili jambo halifiki kokote ni mbwembwe tu au wapo watakaokulinganisha na walioshindwa ilihali tu uache..Sasa kama una moyo mdogo utaacha.
√Pesa nazo zimekuwa tatizo.kuna mtu unakuta ana wazo zuri lakini pesa ni mtihani.
√Wingi wa watu wanaofanya jambo kama analokusudia kufanya,labda ni kuuza batiki unakuta mtaa mzima biashara ni hiyohiyo kwa hiyo mtu akiangalia anasema mmh!ngoja niache wafanye wao tu..
√Hofu ya kushindwa hii nayo ni tatizo,unaweza kuta mtu anawazo zurii lakini anasema hivi nikifanya likashindikana nitaficha wapi sura yangu nk..

Leo nina habari njema kwako unayeogopa maneno ya watu..Wakati nakua niliogopa sana kusemwa na wazazi wangu kunijenga walinieleza vitu viwili ambavyo mpaka kesho naviheshimu.
1.Daima hatuwachagulii watu maneno ya kuzungumza kutuhusu.na kwakuwa binadamu hatufanani hatujipangii kuwa ukikutana namimi usemege hivi tu maana ndivyo ninavopenda kusikia.
2.Ukiwa hai lazima uzungumuzwe na ukifa no one remembers anything about you..pia ikatokea umesemwa jambo ambalo si lakweli why should youshake?so kuzungumzwa kupo..
Tukirudi kwenye mada usiogope maneno japo si mara zote utasemwa kwa ubaya..Lazima uwee na uwezo wa kuchuja taaarifa..kina mabaya huja lakini yamelenga ujifunze,ubadilike na uchukue hatua.Jitahidi usiruhusu maneno yakutoe kwenye ndoto zako.Ukisoma Nehemia 4:3 huyu baba alipata upinzani wa maneno alipotaka kujenga ukuta wa Yerusalem na akaambiwa kwamba hicho anachojenga akipanda mbweha mbona kinabomoka lakini hakukata tamaa aliujenga mpaka mwisho.

Pesa ni jawabu lakini si mara zote,jitahidi kuwa mbunifu kwa sababu ukijiwekea mpaka niwe na hela ndio nitafanya at times utachelewa.

Kwenye eneo la hofu jijengee imani binafsi maana wewe mwenyewe ukiwa hujiamini hao unaotegemea kuwapelekea kitu chako watakipokea??na pia kwenye kuthubutu ndio kunatupa jawabu na kinaposhindikana mara ya kwanza haina maana uache endelea tena na tena mpaka kikae sawa.

Na ile ya kukuta kitu kimoja kinafanywa na watu wengi isikutishe saana.Ndani ya kila mmjoa duniani kuna tofauti hata ukiangalia magazeti yanaweza kuwa na stori moja lakini kila gazeti litatengeneza kichwa cha habari kipekee ndio maana you can make a choice..Sasa uwe MBUNIFU tafuta kitu chako tofauti..Last year mwanzoniii nilikuwa nauza ice cream na tulikuwa watu wanne selling them in the same school nikawaza hapa ili niuze what do I do..nikagundua nibadili aina ya sukari,vifuko,nikawa siweki rangi na size nikaongeza na wakati natengeneza I pray for it na pia kabla sijaenda kuuza naomba pia ..



Guess what kila nikipeleka nilikua nauza zote na watoto wanataka tena..na kupitia shughuli hiyo nilipata pesa zilizozaa ajira maana wakati nipo bize na Ice crem nikapata kazi Tanga so Icecream zikanisponsor  hiyo ajira ya Tanga nayo ikanipa pesa,,mpaka wakati wa kurudi chuo unafika I had a lot of cash namshukuru Mungu.

Songa mbele usiogope vikwazo
ukikuta kizingiti penya mpaka kielweke.

No comments:

Post a Comment