Friday, January 31, 2014

Ladies

Jana kulikuwa na lile swali la je ni sahihi binti kwenda kwa boyfriend na kufanya shughuli za hapa na pale kama kupika,kufua na mengineyo..












SI 

SISAWA!!
kwa binti kuyafanya haya ilhali hujaolewa wala kutolewa mahari na kijana huyo haijalishi unampenda kiasi gani na amekutendea mema kiasi gani..Ikiwa wewe ndiye mke wake mtarajiwa akusubiri tuu wakati ukifika mkaoana utayafanya hayo yoote..Lakini akijua pia anaoa mke na si kijakazi au mtumishi.
Kutokana na shuhuda za watu.wapo waliowahi kujituma hivyo na wanaume wakaoa watu wengine kabisaaa..

Ukisoma 2Samuel 13 Inaelezea binti aliyebakwa na nduguye kutokana na huduma aliyomtolea kaka huyo Amnoni alimpenda sana binti na aliona njia ya kumpata ni kujifanya anaumwa ili binti aje kumletea chakula,wameeenda weee siku ya siku binti akabakwa..

Unaweza kwenda kwa lengo la kufanya shughuli zako na baadaye ukabakwa hautakua na wa kumlaumu as long as you went on your own.
Actually you don't have to prove to anyone that you arr a wife material..A man with respect will wait for you untill its time then uonyeshe all the skills you have.
Take time pia in Proverbs 31 utagundua kitabu kinaelezea sifa za mke mwema so hayo yanayofanyika before wedding si sahihi kwa maana yanafanywa in a long timing though ni majukumu ya kike..

Ladies tupende kwa moyo na kwa akili pia...
Usijirahisishe...
Mwanaume anayekupenda atakuheshimu na kuwa mvumilivu..akianza kuyahitaji mambo ya kwenye ndoa na kwa haraka hivyo weka alama ya mkato na muulize Mungu vizuri..
Pia tuache tabia ya kuwa so demanding kila kitu unamuomba mwanaume mpka na yeye akiamua sasa leo njoo ufue jeans na kusugua sufuria huchomoi yaani..
Nafikiri yale tunayoweza kujitegemea tutatue wenyewe ili isiwe lovetrading..I give you this and you give me that.

Ladies my prayers are with you....

No comments:

Post a Comment