kulikuwa na waimbaji kama Lugano Mwiganege,Leah Amos,The comforters na blogger Natalie Nkya nilikuwepo pia..
Waalimu wa masomo hayo alikuwa ni
1.Mwl.Philipo Sanga aliyefundisha kuongozwa na Roho na kuyajua Mapenzi ya MUNGU..
2.Mbuto Chibwaye aliyefundisha ujasiriamali na kanuni za kufanikiwa kibiblia.
3.Pastor Christopher Mlaponi aliyefundisha somo la uchumba hadi ndoa...
Semina hii iliyoandaliwa vyema ilianza saa tatu kwa praise na worship,baadaye kikundi mahiri cha kwaya ya Casfeta tawi la mlimani maarufu kama The comforters kuimba na baadaye blogger.
Baadaye mzee wa kanisaWilliam Komba akaifungua semina hii kwa maombi na hatimaye mzungumzaji wa kwanza kama nilivyopanga hapo juu akashiriki nasi kile alichokiandaa.
Baada ya semina kuisha tulipata fursa ya kushiriki chakula cha pamoja na siku ikaisha murua kabisa.
Nitajitahidi kuweka masomo yote humu hata ka muhtasi ili wapenzi wa blogu hii mpate vitu vya kuanzia mwaka si ndio enheee.
Nawapenda saaaana.
No comments:
Post a Comment