Tuesday, January 7, 2014

Wema huwa hauozi,,Fred Hammond ni ushuhuda

Fred Hammond ni moja ya waimbaji maarufu sana wa nyimbo za injili huko nchini Marekani na dunia nzima kwa ujumla.
√alizaliwa Tarehe 27.12.1960 huko Detroit Michigan.
√anajishughulisha zaidi na vocals,bass guital.
√akiwa kwenye kipindi cha Donnie Mc Clurkin alitoa maelezo ya huzuni sana jinsi mama yake alivyokiri miaka mitatu kabla ya kifo yake kuwa alitaka sana kuitoa mimba ya Fred lakini ikashindikana na hakujua angemuua mtumishi wa Mungu ambaye ameubariki umma hasa kwa nyimbo zake kama This is a day,everything na No weapon uliovuma sana.


Lengo la kumzungumzia Fred ni huu ushuhuda alioutoa kwenye account yake ya twitter na facebook..Akisema NI MUNGU tu.....
Miaka 23 iliyopita akiwa anaanza muziki hakuwa na kitu na hakuwa na msambazaji wa kazi zake kwa hiyo aliandika namba yake ya simu nyuma ya Cd zake...anasema enzi hizo walikuwa wakilala chini yeye na mkewe Kim na mwanae wa miaka miwili alikuwa akipigiwa simu sana mpaka baadaye akaset mashine iwe inajibu..
Anaukumbuka usiku mmoja akiwa amechooka simu ikaita vijana wawili wakampigia wakajitambulisha wao ni wanachuo wana miaka 17  wamekuwa wakipiga mara nyingi na wamekuwa wakifurahia kile kimashine kinavyojibu..Fred akacheka sana akasema leo ni mimi si mashine wale vijana walifurshi ..dipo Fred akawatia moyo wasome kwa bidii na kuendelea kumpenda Mungu basi vijana wale wakaendelea na maisha yao ila hawakuacha kuwa mashabiki wa Fred..
Wakiwa na miaka 40 sasa mmoja wao alikutana na Fred akamkumbusha ushuhuda huu,akamwambia tumesikia pia kuwa Fred wewe ni mgonjwa na unapaswa kufanyiwa operesheni magoti yote sasa ni hivi yule rafiki yangu mwingine ni daktari bingwa na ana clinic yake ya mazoezi.Ndiye huyo aliyemhudumia Fred  na hakumchaji hata senti moja na sasa Fred anaendelea vizuri na shuhuda hii aliiandika wakati anafanya mazoezi  yake...

Nataka tujifunze haya
1.tusiwatendee wema wale tu tunaowajua yakesho hatuyajui...tunaowaona hawafai leo pengine wakawa mfano wa oxygen tunayoilikia daily Mungu asitunyime..angalia sana namna unavyojibu,na kuwatendea wengine.mwenzetu angewatukana au kuwasema ovyo angeharibu reputation yake kwa jamii na hata kuufunga muujiza huu wa uponyaji.
2.wema huwa hauozi..tuendelee kuwafanyia watu wema tutavuna kwa wakati tusipozimia mioyo.Fred alipanda wema huu kwa vijana hawa wakiwa na miaka 17 na amekutana nao wakiwa na miaka 40 hebu fanya hapo mahesabu uone Mungu alivyo waajabu.

Endelea kubarikiwa na kuwa baraka kwa wengine.....



No comments:

Post a Comment