Wednesday, January 8, 2014

Breakfast is important.

Ni siku nyingi sana hatujagusia kipengele cha afya  si ndio enhee.

Leo ngoja tuangalie umhimu wa kifungua kinywa maarufu kama breakfast..Kila familia au mtu binafsi ana cha kwake mwingine atapenda apate supu ya nguvu,Chai ya nguvu na vitafunwa vyovyote au uji nk.
Kila mtu ana chaguzi lake lakini kitaalamu kadri Mungu anavyotupa uzima na uwezekano wa kupata kifungua kinywa tusiache tumbo wazi..
Kitaalamu wanasema ule muda toka usiku mpaka asubuhi ni mrefu sana na kuna vitu vingi vinakuwa vimeendelea kwenye mwili hivyo kuuacha tena bila kuupa cha kuushitua si sawa..

Tuzipitie sababu za kwanini Breakfast ni muhimu.

√inakusaidia kuianza siku vyema na hata kuimaliza maridadi kabisa kwani itakupa changamko.hakuna asiyependa kujisikia vyema au anayependa kuwa na nusu furaha..Hivyo basi unapopata mlo huu hukufanya uchangamke na kuifurahia siku yako na kuwa si productive.

√Hutupa msawazo wa akili(concentration)katika lolote la siku husika.

√Huipa miili yetu virutubisho..

√hutengeneza mood zetu..mwili ukikosa changamsho lasubuhi ni rahisi mtu kuwa irritated hata kwa jambo dogo..

Tujitahidi sana breakfast is giving us more mental advantages..kwa wale wanaoskip hii kwa sababu zao binafsi it is not supported at all.

kama ni mzazi hakikisha mtoto kabla hajakwenda shule unampa kifungua kinywa.

#hebu share nami breakfast yako huwa ni nini kwenye nadonjob1@gmail.com

No comments:

Post a Comment