Saturday, January 4, 2014

Kuna tumaini JIPYA kila wakati na kwenye kila hali..CHEER UP..


maisha yetu hapa duniani ni kama safari unapotembea unabadili mazingira(jiografia),kuna sehemu utakuta milima na wakati mwingine mabonde,miiba na michongoma.Kwenye safari hiyo utakutana pia na majira tu kuna wakati utafurahi,utalia,utafanikiwa na kushindwa pia..
Ninajua unavyohisi
√pale unapotengwa na wengine kutokana na majira unayopitia kwenye maisha.Kuna marafiki watakupenda kwa sababu ya ulichonacho au hata mazuri uliyonayo lakini ukifika kwenye utelezi wanakuacha woote.
√pale unaposingiziwa na kuchunguzwa kwa siri na watu walioweza kuja kwako mojamoja na kupata ufafanuzi..
√pale unapoaibishwa na mtu kwa makusudi ili yeye aonekane mwema..
√pale unapowapenda watu,waheshimu ila wao wanaamua kuweka moyo na heshima yako at the bottom of their shoes.
√pale mambo yanapokwama na kurudi kwenye sifuri..huku kila mbinu unayoweka inakwama.
Napenda kukupa ukweli huu haijalishi una-feel nini THERE IS ALWAYS A HOPE...
kama utaamua kutoka ndani kuamini kuwa jua litawaka tu siku moja na haya niliyonayo yatayeyuka kuwa historia..Itakuwa hivyo
chochote unachokisafiri leo hapo kwenye maisha yako kuna walimwengu billioni wamekivuka na maisha yao yameendela mbele.
Zaburi 23:4"Naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,sitaogopa mabaya;Kwa maana Wewe upo pamoja nami,gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Hizo ni ahadi za Mungu kwako
1.haijalishi bonde gani huwa hatukai hapo milele ni kukutana nalo nakulipita.Uwe na moyo mkuu kila changamoto uliyonayo hukai nayo milele UNAPITA tuu.
2.hauko peke yako Bwana yuko pamoja nawe bega kwa bega and at the end of the day ndiye mfariji..

Wish you nice weeked..
victory is yours no more pain this year..


No comments:

Post a Comment