Wednesday, January 1, 2014

arise above that background and be better not bitter

Maisha haya yana mambo...
Tunapozaliwa hatujichagulii tutaishi vipi na kukutana na yapi.
kila mtu ana background yake,
√yupo aliyetoka kwenye familia ambayo ameona baba akirudi asubuhi na kumpiga au kumtukana mama na wao watoto wasisemeshwe kwa upendo au hata kuulizwa mahitaji yao.
√Yupo aliyelelewa na mzazi mmoja.kwa kuambiwa mzazi mmoja alikimbia au kufariki..
√yupo aliyezaliwa hapendwi tu pasipo hatia yoyote..
√yupo aliyetoka kwenye familia ambayo neno nakupenda,pole,hongera ni msamiati mkubwa kwa sababu hajawahi kuyasikia.

Haya na mengineyo yana madhara makubwa sana kwenye maisha yetu ikiwa mhusika hatachukua hatua ya kuyashinda ana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa.kuna watu leo hii wamekuwa wezi,wauaji,walevi,wachoyo,wachafu,makatili kutokana na background zao..

Siifahamu background yako lakini nataka nikutie moyo upo uwezekano wa wewe kuishi maisha mazuri tofauti na hayo uliyopitia..nikiwa shule baadhi ya rafiki zangu wakike walikuwa wasafi sana na wanaofanya kazi za mikono vizuri sana mpaka leo wako hivyo lakini baada ya kukaa nao walinambia mama zao walifariki wakiwa wadogo hivyo wamejilea zaidi wenyewe na  kwa mateso zaidi kutoka kwa ndugu zao.
hili jambo lilinipa funzo mimi ambaye nina wazazi wote kuwa kama hawa na background yao wamejifunza haya na wako hivi vipi mimi.
√amua binafsi kupaa juu ya background uliyonayo..
idhibiti kifikra kuwa niliteseka sawa lakini future yangu haina sababu ya kuendelea kuwa ya mateso au ya maumivu,Mimi ..... nitakuwa chachu ya mabadiliko katika familia hii na ukoo huu.
√unapopata muda kataa zile (spirit)au roho za mambo ya kale kutofuatilia maisha yako.kuna vitu vipo ni laana au vya kurithi kwenye familia na koo tulizonazo sasa bila Mungu kutoa tamko la kukomesha itaendelea hiyo hali milele na hutaweza binafsi kuihandle.
√tafuta mafundisho yanayoziba lile pengo au ufa ulionao kwenye maisha,jifunze pia kwa watu pia waliovuka kutoka kwenye background kama uliyonayo na kufanikiwa.
mfano:umetoka nyumba ambayo hautiwi moyo,haupongezwi na wewe ungependa kuwa na ndoa ambayo utawatia moyo wanao.Jitahidi kusoma vitu hivyo  viishi,na eventually utashangaa mtazamo wako unabadilika.
Nimekupa mifano mingi kwenye post zangu za watu maarufu wenye background mbaya na ngumu ila waliamua kupaa juu ya background zao na hatimaye wakaishi ndoto zao na kufurahia maisha.

ninakuombea uwe na ushindi katika yote unayoamua kuyaishi..
√uliyekosa upendo wa wazazi jikumbatie jipende soma neno la Mungu utashiba pia pendo lake na kuwa chachu ya upendo kwa wengine.

√uliyekosa mzazi wa kukuelekeza kazi za mikono au ubinti ,usizubae tu tafuta jinsi ya kujifunza hata kuuliza wengine..so as you become a best mother to come.


ARISE everyone!!!your past is past and it has nothing to do with your future .maamuzi yako mikononi mwako to be better or bitter..


No comments:

Post a Comment