U hali gani?
Natumai umeamshwa vyema na kufanikiwa kuuona mwaka mpya...
natumai pia ulimshukuru Mungu na kuandika mikakati ya mwaka huu mpya..
Salamu za mwaka mpya ni maandiko mawili tu ya Zaburi ambayo yamelenga busara kuu moja nitakayokushirikisha...
Zaburi 27:4"Neno moja nimelitaka kwa BWANA.nalo ndilo nitakalolitafuta,Nikae nyumbani mwa BWANA sikuzote za maisha yangu,Niutazame uzuri wa BWANA na kutafakari hekaluni mwake..."
Zaburi 32:8"Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri,jicho langu likikutazama"
Tunauanza mwaka mpya ni vyema tumpe Mungu kipaumbele cha kutosha yeye awe yote katika yote.
Kama kuna ushauri wa bure ninaoutoa ni kusisitiza UHUSIANO mzuri na Mungu.
√ana sifa ya kuwa mshauri wa kweli-haijalishi ni eneo lipi la maisha,ukijenga uhusiano mzuri nae atakuambia mwanangu hapa sawa hapa hapana kwa nini usifanye hivi...mahusiano yako,ndoa,ajira,masomo yakisimamiwa na Mungu utakuwa ni mwenye furaha..
√ana sifa ya uongozi-atakuambia katika hii mipango uliyojiwekea anza na huu,mshirikishe fulani au una tatizo hili muone fulani atakupa neno la kukujenga na kukuimarisha na utashangaa kama mtu yule uliyeongozwa kumuona mkikutana atakupa mifano exactly na jambo lako au hata kukwambia yeye alivukaje hapo.
√Mungu ni mfariji wa kweli-hakuna kumbatio la kukupa changamko la moyo kama linalotoka kwake,nakumbuka kila ninapozidiwa na mambo ninajiachia kwake na kumwambia Mungu nikumbatie and I can feel his presence,his touch and so much more..pale faraja ya wanadamu inapofika kikomo Mungu anaingilia kati..Isaya 41:10.
Nikutakie mwanzo mwema wa mwaka.
palilia uhusiano wako na Mungu kila siku bila kukoma.
Soma neno,pata muda wa kuzungumza nae.uhusiano mzuri unajengwa kwa mawasiliano.unapowasiliana na Mungu kila mara anapata fursa ya kukuambia vitu vingi vya kukuhusu lakini unapomtafuta kwenye shida tu hainogi...
Love you all.
Tuanze na Mungu in all aspects of life..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment