Tarehe 11Disemba ni siku ambayo hunipa faraja na kuniongezea nguvu kuendelea kupambana na kumpenda na kumtumikia MUNGU na wanadamu wenzangu.
Ilikuwa usiku wa kuamkia tarehe 11,nikiwa natoka maombi ya fellowship rafiki yangu akaniSMS kuwa tuna presentation darasani ningependa part ipi maana tulikuwa group la watu kama kumi na tano hivi,nikamjibu nipeni tu Conclusion,akasema hayatukutane kesho.Nikiwa njiani nikasikia ndani ya moyo wangu sauti "Natalie kaandae presentation nzima hujui kesho nini kitatokea"hapo ni saa 6usiku nimechoka sana.
Nilitii nikaandaa then nikalala
asubuhi ya presentation ilifika cha ajabu mwalimu yule hakuwa mwenye ukali,, ila siku hiyo alikuwa mkali sana alipotuona alifoka tu akatuchallenge tulivyo na baadaye akasema hebu anzeni presentation,tukaanza ghafla akahamaki"hiki kikundi hakipo serious na nitawapa ziro"
kusikia vile mwe nilichoka nikawa naomba moyoni nikasema"Mungu kwa hiyo ulivosema niandae summary kama mnavyoiona hapo juu kwenye picha ilikuwa ya nini?,na hiki chumba cha presentation mimi nilikuwa kiongozi for two years kwahiyo ndio unaniaibishia hapa?na hii ziro ndo ya kwangu mlokole mzima kati ya darasa hili la watu mia 2?
baada ya pale nilimsogelea Mwalimu nikamwambia nitapresent kwa niaba ya watu woote hawa,akaniangalia juu mpaka chini nikamwambia "ndio mimi nitafanya hivyo."
nikaanza kufanya kabla sijamaliza akanikatisha"wewe ulikuwa wapi,umesoma wapi maana toka naanza kazi,sijasikia presentation nzuri kama hii YOU ARE THE BEst student of this year for the course and an exempler student "you are smart,intelligent na masifa kibaoo.moyoni mwangu nilinyamaza nikajua ni MUNGU wa kuchukua sifa hizi zote so nilinyamaza akasema tena kwa hili nitaondoa ziro nitawapa B+ na mnapoleta kazi mmtaje huyu binti niongeze zaidi.
The class was over wenzangu wakaja kunishukuru and was telling them guys its not me it is GOD kila mtu akamshukuru Mungu!! I never did it I was just a vessel.
Ninambariki Mungu wale rafiki woote ni graduates now but huniambia Natalie utabaki mioyoni mwetu for your kind deed.
Siisahau siku hii kwakuwa moyoni mwangu napenda kusaidia wengine kwa presence yangu kwenye maisha yao,ili nao wafurahi na kumuona Mungu kupitia mimi so nilifarijika kujua Mungu yupo kazini nami masaa 24,kila nikikumbuka hili nalia kwa furaha na kumhofu Mungu, na hunitia nguvu sana kuishi kwa ajili ya wengine..
Funzo ni:
√kwa eneo lolote ulilopo wewe ni balozi wa Mungu kuna jambo unapaswa kufanya kwa wengine.
√ikiwa ni kazini ,shuleni hauko hapo tu kama upo ila kuna jambo zaidi ya hilo.Mungu akusaidie ulifanye.
I Glorify GOD kwa hili utukufu wooote auchukue yeye mimi nitaendelea kushuka chini illi yeye ainuliwe juuuu.
No comments:
Post a Comment