Monday, December 9, 2013

Ladies lets bargain and reach reasonable solutions!!!

Kama mabinti tunakumbana na changamoto nyingi hasa tunapotaka kutimiza malengo na ndoto tulizonazo,tutamuomba MUNGU sana na kulia machozi mengii lakini kuna wakati unapaswa ujifunge kibwebwe HAPANA yako iwe hapana na usimamie maamuzi yako.
√wengi tumeharibu maisha yetu kwa maamuzi ya dakika chache na kuishia kuwa wenye majuto.Niliwaza jambo hili ikiwa ukienda dukani ukataka kununua nguo ya thamani sana au kusuka nywele za bei fulani utalalamika mpaka itapunguzwaa au wakikataa basi unaondoka na jibu huwa kama leo imeshindikana nitanunua wakati mwingine.
Imekuwaaje sasa kwenye mambo yanayogusa maisha yako unazubaa bila hata kubargain,unalazimishwa kufanya mapenzi ili usaidiwe mtihani au wimbo wako utoke studio na wewe unakubali pasi na kubishana au kukubali kwenda kujituma mwenyewe kwa kujisomea ili ule matunda ya jasho lako,au kusubiri milango mbadala wa kutokea kwenye ndoto zako.

Nikiwa binti pia nazielewa fika changamoto tulizo nazo ila wanaume hawawezi kutuheshimu ikiwa tunafungua milango kirahisi na kushindwa kusimamia mamb fulani yanayogusa maisha yako wewe binafsi kama binti.Maneno ya Mungu yanazungumzia kupewa akili na Mungu so kuna mambo yatakutaka utumie AKILI kuyahandle,yawezekana ulijinyima msifanye mapenzi akakuzidi nguvu mbona sasa anakushauri mfanye abortion unalegeza masharti na unakaribia kukubali.
√lets wake up sisi ni vyombo vya thamani vinavyotegemewa na Mungu,familia zetu na taifa hili.Tujifunze kusimamia mambo yetu mpaka yatokee njia za shortcut hazitatusaidia maana zitatuandalia majuto na maumivu tu.
•upo shule:kazana acha uvivu na kujilengesha upate marks za bure.
•upo kazini:chapa kazi huitaji kuutumia mwili wako kuongeza vyeo acha uwajibikaji wako uwavutie watu wakupandishe juu.
•una ndoto zako:si kila mkono utakaokunyookea uliko unataka kukusaidia kaa chini muulize Mungu usiwe na pupa ukijipa nafasi utagundua ni wa halali au fake.

#ninakuombea upate akili katika mambo yote na hata kama ulikosea neema ya Mungu bado ipo sana kukusaidia na utavuka kwa ushindi mkuu sana.
pokea ujasiri katika jina la Yesu wa kusimamia maamuzi yako na kuyatekeleza.


No comments:

Post a Comment