Friday, December 6, 2013

Chonde kina baba na kina kaka!!!"

Leo nizungumze na kina kaka na kina baba,,
wakati wanaharakati,serikali,vyombo vya habari na hata dini zikihubiri kuhusu kumkomboa mtoto wa kike kielimu na kimaendeleo,wenzetu baadhi(kaka,baba)naona kama mnatupinga kwa sehemu fulani kutokana na haya mnayofanya.
√wakati wa usaili waajira badala ya kuzingatia wasifu wa muombaji mpo wachache mnaoomba rushwa ya ngono ili hiyo nafasi ipatikane sasa hiyoo kazi ikipatikana mnaendeleza mahusiano ya kimapenzi au kufanya kazi??
√kwa wale walioko mashuleni au vyuoni ili maksi ipatikane au fidia ya test mtu alizokosa zifanywe! binti lazima atoe hongo ya ngono ili hilo tatizo lisuluhishwe.
√kwa wale maarufu au wenye nafasi zao nyeti na muhimu kwenye jamii hutoa masharti magumu yanayoashiria uhitaji wa mahusiano ya kimapenzi ili tu msaada utolewe mbaya zaidi mpaka makanisani haya mambo yameingia,ili dada alead praise au aachiwe mic shurti atoe ngono kwa mjoli ndipo nafasi itolewe au kaenda studio kuandaa album wembe ni ule ule.
√wengine ni watu wazima kiasi cha kuwa wazazi wa mabinti hao,lakini badoo atatoa pesa zote ili kumhadaa binti na hatimaye kumvunjia au kumharibia ndoto na malengo yake,kwa ofa za hapa na pale..

Ndugu zangu tuungeni mkono kuwatia moyo mabinti kuzitimiza ndoto zao na si kutumia nafasi zenu au mlivyonavyo kuharibu watu ambao wangekuwa lulu kwa taifa na kanisa.
Naamini nafasi au kipato ulichopewa si cha kukomoa wengine na kuwaumiza naamini ipo sababu ya msingi ya wewe kuwa baraka kwa wengine.
Vitumie ulivyonavyo kwa utukufu wa Mungu.

No comments:

Post a Comment