Ladies:
baada ya kumuomba sana Mungu kuhusu kupata mwenzi.kuna kitu tunasahau na si vibaya ukakiombea pia,hiyo familia mpya unayoenda kuishi nayo,maana biblia inasema 'utaacha wazazi wako na utaambatana na mumeo'.Ina maana unaenda kuwa na wazazi wapya na ndugu wapya na taratibu mpyaa si vibaya ukatamka neno la utangulizi kama mwana wa Mungu.
Hebu tupitie neno la Mungu linalohamasisha kumuomba Mungu kwa mambo yajayo(ISAYA 45:11a)"Bwana,Mtakatifu wa Israel,na Muumba wake,asema hivi;Niulize habari za mambo yatakayokuja;
√Omba kibali huko unakokwenda.Mara nyingi tumeona mikwaruzano kati ya mawifi,mara mama mkwe,lakini maombi ya mapema yatakufaa kukuandalia njia huko uendako(ISAYA 41:21)
√Omba ukafanyike baraka,yawezekana ukaolewa pahali wewe tu na mmeo ndio mliookoka hivyo wewe unapaswa ukawe chachu ya wokovu huko ukweni.(RUTH2:11).
√Ikiwa Mungu amekupa neema ya kuifahamu familia hiyo kwa uchache ombea vitu vya msingi unavyojua na kataa kama kuna laana za ukoo,magonjwa ya kurithi,matambiko n.k sasa kama binti yaombee haya mapema kwa amani(YEREMIA 1:10)
Omba na mengine mengi kadri Mungu atakavyokujalia na pitia kitabu cha Ruth kuna mambo mengi ya kujifunza ,kiri ushindi wa ndoa nzuri na yenye mafanikio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment