Harufu ya kinywa au Helitosis kwa kizungu ni matokeo tu ya uwepo wa bacteria au mabaki ya vyakula kwenye kinywa ndio maana ukiamka asubuhi harufu ya kinywa haivutii hata kidogo.
NJIA HIZI ZITAKUSAIDIA uwe na harufu nzuriii:-
1.Safisha ulimi-unapopiga mswaki usikazane kwenye meno wee,safisha ulimi japo kwa dakika kadhaa.utaondoa mabaki ya vyakula na hao bacteria waharibifu.
2.Acha kinywa na unyevu-a dry mouth stinks,na ndio maana ukiamka asubuhi unasikia harufu kali maana kinywa kinakuwa hakina mate na ni mate yanayosaidia kuondoa bacteria na mabaki ya vyakula,kunywa maji ya kutosha kuchochea unyevu.
3.Tafuta chewing gum hizi zitakupa harufu nzurii na pia zinasukuma ongezeko la mate kwenye kinywa ambayo tumeona yanahitajika.
5.Jenga pia desturi ya kubadili miswaki mara inapochoka.
#ukifuata mbinu hizi ukashindwa kupona muone daktari kwa msaada zaidi#
No comments:
Post a Comment