Wednesday, December 11, 2013

Kama Mama huyu aliweza unaweza pia!!!!

As life goes on and on kuna wakati unakuta mazingira yamekubana mpaka unaona ndoto ulizonazo hazitakaa kutimia milele,ashukuriwe Mungu ambaye huingilia kati pale akili zetu zinapofika ukomo na kuturudishia nguvu kama tai na hivyo kufanikisha tunayotamani yatokee.
Leo nitakukutanisha na rafiki yangu Jane  Macha ni mama wa watoto wanne aliyefanikiwa kujiendeleza kutoka u-nesi wa daraja la chini mpaka kuwa PHD holder.Amekuwa pia mchapakazi sana hivyo kugombewa na mashirika ya afya hapa nchini na nchi jirani.


√Jane anasema alianza kazi kwenye hospitali ya mkoa akiwa nesi wa kawaida sana,alifika mahali alichoshwa na kazii hi na alitamani sana ajiendeleze kielimu,akaanza kusoma kidogo kidogo hapa nchini na baadaye kwenda nje kumalizia PHD.
√Siri kubwa ya mafanikio yake ni kutokukiri au kukubali kukatishwa tamaa maana anasema alibezwa sana ,we nesi unataka kusoma utaweza kweli??lakini yeye alitazama dhamira yake ya ndani kwamba licha ya maneno haya mimi ninataka nini???
√Pia maombi ni sehemu ya vitu vilivyompa kushinda,alimpa Mungu nafasi ya kumuelekeza afanye vipi mambo yake,na alidumu kumtolea sadaka pale anapomvusha kwenye masomo yake.

Na wewe pia unaweza kuwa chochote unachotaka kuwa ukiweka dhamira ya ndani kwamba iwe iwavyo na Mungu akiwa upande wangu nitafanikisha tu ninayoyatamani.
Usikubali au usiruhusu maneno ya watu yatie giza kwenye mikakati uliyonayo.
Mtegemee Mungu,pambana vilivyo upenye.Watu wote waliofanikiwa kama Jane walichukua maamuzi magumu,kuna mambo utatakiwa uyaache kufikia unakotaka,kuna watu itabidi wapungue ili usonge mbele.
Acha kujipa visingizio nimetoka familia maskini sijui nini na nini.Mungu huitazama nia ya mtu halafu hufungua milango ya kukufinance ndoto yako.apart from that utabaki tuu kulaumu.Jane akuhamasishe kwa leo.

#much love to you all.#

No comments:

Post a Comment