Paula White ni mwanamama role model ambaye analitumia neno la Mungu ipasavyo kurudisha nuru na mwanga kwa maisha ya watu pasipo kujali hali zao.
√Paula amezaliwa 20.4.1966 huko Tupello USA.
√Paula ni mchungaji,mwalimu,mwandishi na vitu vingi.
√Paula ni mama wa mtoto mmoja kwenye ndoa yake iliyodumu kwa muda na kukatishwa ghafla.
Akiwa na miaka mitano baba yake mzazi alifariki hivyo kuwaacha kwenye malezi magumu yaliyojaa umasikini mkuu baada ya muda iliwalazimu kuhama walipokuwa wakiishi na mamayao,hapo matatizo ndio yalipoanza alipatwa na udhalilishaji wa kingono akiwa shule,akaja kupata ndoa ya utotoni ambayo haikudumu ilikuwa ni mwaka 1984.
Anasema alikuwa kwenye maumivu sana(betrayal,confussion,abandonment)mpaka siku moja akiwa na miaka 18 alipokwenda kanisani akakutana na wokovu,siku moja aliinua biblia juu akasema"God I don't know you and i don't know even myself but i know the answers are in this book"baada ya ukiri huu akanza kumtumikia Mungu.
√Mwaka 1990-2007 aliolewa tena na Randy mwanaume huyu ambaye pia ni mtumishi wa Mungu hawakudumu kutokana na vitendo vya kinyanyasiaji alivyomfanyia anakumbuka wakati mmoja Randy alimfunga kitambaa usoni na kumfungia kwenye chumba chenye giza bila msaada kwa masaa kadhaa.
hayo yakiwa yanaendelea rafiki yake aliyempenda sana akabambikiwa kesi na kufungwa jela.
kidogo tena mwanae wa kiume akaathirika na madawa ya kulevya na kufanyiwa udhalilishaji wa kingono na mmoja wa wafanyakazi wake wakiume hapo ofisini.
hakukaa sawa binti wa mumewe Randy akafariki kwa brain cancer wakiwa tayari wamedivorce.
wakati hayo hayajaisha akaingia kwenye kashfa ya kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Benny Hinny anasema alikuwa na wakati mgumu sana lakini alikataa kukata tamaa na kumuishia Mungu akiamini shetani alikuwa akipiga vita huduma yake.
Unaweza kujiuliza amewezaje kuwa na ujasiri licha ya majaribu yote haya??i dont know what your facing but dont give up Yohana 16:33 Yesu anasema duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo nimeushinda ulimwengu.
Nimeshare nawe story hii kukutia moyo haijalishi unapita kwenye gumu gani linda kile Mungu amekiweka ndani yako.unaweza kuumia lakini kila tatizo lina death date yake...endelea kumpenda Mungu hayo yote yatapita kama moshi...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment