Thursday, October 19, 2017

Namna bora ya kusubiri

NAMNA BORA YA KUSUBIRI


 Hakuna anayependa KUSUBIRI hasa katika karne hii ya mambo ya shaa shaa/ fasta fasta( A microwaved kinda generation)
Wewe ni shahidi unavyokereka kusubiri foleni bank,taa zinazoruhusu magari barabarani au hata mhudumu anapokucheleweshea chakula/ kinywaji chako!! Kwa Mungu ndio huwa hatumuelewi na tunaumia haswaa!!!pale alichoahidi kinapokawia au unaloomba na kuhitaji kwa sana linapochukua muda kutimia

Kwenye kusubiri suala huwa ni namna gani tunaweza kusubiri na si kama inawezekana/ tunaweza kusubiri!!
Kwenye maisha kuna vingi tunavyohitaji au hata kutamani Mungu atupe lakini haviji paap naongelea zaidi vile unavyoweza kungoja!!
Hutupelekea kumuona Mungu hakuwa in control na haoni uharaka wa hitaji letu!!

Si kipindi kizuri maana
* Moyo huchoka na huumia sana kwani sauti za kujilinganisha na wengine huimba sana!!
* Kujikatisha tamaa au hata kukatishwa tamaa na wengine hujitokeza!!
* Hutufanya tutupe tumaini na tegemeo letu kwa Mungu na hapa ndipo mawazo ya kutafuta njia fupi huja!!

Leo nataka tumtazame Daudi kupitia Zaburi 27 yeye alikuwa ni kijana ambaye alikuwa ametawazwa kuwa mfalme katika umri mdogo sana kama 16 hivi lakini alikutana na mambo magumu mno na iligharimu miaka 14 baadaye ndio akawa mfalme kamili... alipata maadui wa kumtosha alikuwa na mategemeo,matumaini na matarajio kwa Mungu lakini hayakujipa siku moja yalitokea baadae!! Aliumia sana na kulaumu lakini alikuwa na IMANI ipo siku Mungu atabadilisha historia yake na kuleta shwari kuu!!

Mtu mwingine ni Ibrahim nae alipita katika kipindi cha kusubiri baraka yake ya mtoto!!
Ulikuwa ni mtihani kidogo,,huyu ni mtu anayesifiwa kama Baba wa Imani lakini naye alipwaya katika kusubiri. Alifika mahali akaona atafute njia fupi katika kupokea hitaji lake ambalo liliigharimu ndoa yake!

Kusubiri kunachosha na kuna maumivu mengi lakini mara zote Mungu alipochelewesha mambo yetu hulenga
1. kutufundisha uvumilivu na hufunua tabia yetu halisi!!Ni kipindi cha kusubiri baraka za Mungu ndipo utajua tabia yako halisi na hata kujifunza uvumilivu na mengi ambayo Mungu anataka ujifunze kupitia hitaji lako!!
2. Hutufunza namna ya kuweka tegemeo letu kwake na kumtegemea!!
3. kutuandaa kubeba jambo hilo ambalo analiandaa kutupatia, hutusaidia kubeba jambo hilo kwa nidhamu na uthamani kutokana na uzito tuliokuwa nao wakati wa uhitaji nk....
Hapa  nitatoa mfano wangu binafsi kwa miaka zaidi ya 20 nilikuwa na tatizo la sukari ya kushuka na moyo tatizo lililokuwa limenisumbua sana nilikuwa naamini kuna siku nitapona japo kuna saa hali haikuwa inaonyesha nitapona,, Nilipokuwa nikizidiwa na kuona kama leo ndio inakuwa mwisho wa uhai wangu nikawa nasema Mungu utaniponya lini? nachoka kusubiri,,mbona naombea wengine wanapona mie bado? neno lako lina ahadi nyingi mbona hunitendei?nadhani nitakuwa makini na afya yangu maana anytime I can loose it!!
Yeah I got better after waiting for a very looongest time na nikajifunza kuheshimu uhai wangu sana, hivyo kila siku ninapoamka mzima inanipa kuona namna nilivyo si kwa  nguvu au uweza wangu ila ni kwa huruma za Mungu!!Maana yeye ndiye hutoa uzima na anaweza kuchukua muda wowote na nikagundua kule kusubiri kumenipa nidhamu kwa Mungu na kwa jambo alilotenda!!

Sasa ni vizuri kuelewa kila anacholenga Mungu katika jambo unalosubiri maana usipoelewa kila hatua hapo lazima upige maktaimu mpaka mambo yakae sawa ndipo uhitimu na kupokea muujiza wako!!

Kuchelewa kwa jambo lolote jema huwa kumefungwa na ukuu wa kiungu ndani yake sasa likija nusu au bila ukamilifu wake litasumbua tu!! Hivyo ni aheri kusubiri..

  Sijui unasubiri jambo gani naomba nikutie moyo kusubiri katika Mungu!!
Yeye ni mwaminifu sana atatenda kipo anachotaka ujifunze kwake na kipo anachotaka kitendeke ili Yeye atukuzwe kupitia maisha yako VUMILIA

Tutaangalia namna bora sasa ya kusubiri!!
Kwenye sehemu ya mwisho ya somo letu

    Itaendelea........,

Tuesday, August 22, 2017

Daima jipende kwanza!!

#AndSheRemberedHerWorth
#ChooseDay
#NoMatterWhatChooseYOU
#ItsneverSelfishbutSelfLove

What puts us women in troubles is loosing ourselves in moments or acts of kindness or passion beyond our ability!!At times unknowingly that moment offers more power to someone to abuse you!!Until you realise that you have wasted time and so many things!!
Self worth is never a bartery trading that you offer s.th of your own to be accepted/appreciated/recognised/loved etc!how you handle/treat/carry yourself and your issues speaks volumes!!

              Mtu pekee anayeweza kuutosheleza moyo wa mwanadamu ni aliyeuumba!!
Woman stop doing the unspeakable in the name of LOVE!!
It's trending nowdays women undervaluing themselves just to keep the man or the relationship!!When you value yourself you will set the standards with grace and elegance!!
Have self love and that is not selfish
At times we perpetuate men to abuse us basing on pretendence of being superwoman while it breaks us and make us unworth!!You can never give what you don't have,,Sasa wewe mwenyewe hujipendi wala kujijali hayo umpayo mwingine mpaka kutaka kuharibu utu wako unayatoa wapi??

Thursday, August 17, 2017

Akaikumbuka thamani yake!!/And she remembered her worthy

Na akaikumbuka thamani yake Part1!!

         Mtu yeyote anayeijua thamani yake hujiwekea  binafsi viwango vya juu vilivyojaa neema na ustadi katika namna anavyoishi na anavyofanya mambo yake!!
Hakuna anayeweza kuwa vyote kwa kila mtu na kuwafurahisha wote anaokutana nao kwenye maisha lakini anaweza kuujua uthamani wake na kuishi kwa staha akifanikisha mambo yake na kuwa mwenye furaha!!
Ni mpaka tu mtu atakapothamini maisha yake na utu wake ndipo atafikia kilele cha kuwa mwenye furaha na kufanikisha mambo yake pasipo kuwanyooshea wengine vidole kama  vicheleweshi au vizuizi vya furaha na kutimiza ndoto zake!!
Jamii nyingi za KiAfrika zimekuwa na mtizamo kandamizi kwa mtoto wa kike/mwanamke kijumla na kadri siku zinavyosogea mambo yanakuwa magumu zaidi hivyo kupelekea wengi kukata tamaa ya kupambania ndoto zao na hata kuishia kuwa wenye huzuni na msongo wa mawazo usiokoma.Sasa kama mwanamke hautaamka binafsi kuitambua thamani yako na kuchangamka tutachelewa sana,maana kila tunapojitahidi kuinuka lazima tuonekane tunatafuta usawa na wanaume au kushindana nao sasa hili si jambo zuri maana tutakuwa na kizazi cha wanawake wanaokalia ndoto na kuwa nyong'onyezi!!
Kama unapita katika hali hizo hebu jaribu kufanya haya:;-

•Linapokuja suala la kuwa na furaha au mafanikio sio sahihi kuweka hisia na matarajio yako kwenye mikono ya mtu mwingine,shauku ya kuwa mwenye furaha au mafanikio inakutegemea wewe binafsi kwa asilimia zote.Imo nguvu ndani ya kila mwanamke ya kuwa bora,kufanya vitu kwa ustadi nk,bila kuitaji maoni ya pili kutoka kwa mtu yeyote na ukilijua hili maisha ni marahisi mno!
1.Angalia ni kitu gani kinakudunisha/kukukwamisha jitenge nacho na ikishindikana kipuuze.Jione kwa namna ambayo Mungu anakutazama kama kiumbe bora na cha maana chenye uwezo wa ajabu kufanya mambo makubwa.
2. Kama uliweka imani yako juu ya watu fulani kwamba bila wao huwezi kuwa mwenye furaha au mafanikio you must take your POWER back si lazima kwa mkupuo anza taratibu kwa kufanya yale yakupayo furaha kibinafsi au vitu vile vilivyo katika uwezo wako kutenda bila mtu wa pembeni.
3. Mwendee Mungu YEYE pekee ndio chanzo cha furaha ya kweli na ndie dira pekee katika kila jambo utakalo kulifanya haijalishi ni kubwa kiasi gani!!Daima yupo kutuonyesha njia

Friday, July 21, 2017

Men of prayer lift their hands to God in prayer but never in beating women to violate/abuse/kill/mishandle them!!
•praying hands are protective!!
•praying hands are assuring ones!!
•praying hands are giving ones!!
So assess your hands today!!

Wanaume waombaji huinua mikono yao kwenye maombi!!Hawaiinui kuwanyanyasa, kuwapiga wanawake au kuwatendea ukatili!!
•Mikono ya maombi ni mikarimu!!
•Mikono ya maombi hutoa hakikisho!!
•mikono ya maombi hulinda na kutunza!!

Jikague leo!!

#AchaUkatili
#SambazaUpendo
#NatalieNkyaSukambi2017

Monday, March 20, 2017

Tukiwa tumebakiza siku kadhaa kwa ajili ya duara letu litakalofanyika Jumamosi hii 25/3/2017!
Naomba kukualika tena binti mwenzangu uje tujifunze pamoja THAMANI YA MWANAMKE pamoja na mambo kadha wa kadha!!
Mahali ni LightHouse Christian Centre (Ubungo) ni karibu na njiapanda ya chuo kikuu cha Dar Es Saalam nyuma ya kota za Tanesko!!
Ukikwama tumia namba Hii 0718664741
Karibu sana sana!!!!!!


Wednesday, February 1, 2017

Simama,Futa machozi,Tazama vyema

SIMAMA
FUTA MACHOZI
TAZAMA VYEMA
WEWE NI SHUJAA
         Woow maneno haya ni ya wimbo mmojawapo wa Angel Benard niliyapenda sana!nikiamka,nikikaa nakutafakari uzuri wa kuwa kwenye sayari hii yenye hewa ya bure ni mibaraka tele,huwa nauinjoi sana!
Haya maneno yakiongezewa vitendo yana nguvu na umhimu sana.Maisha si siku zote hurudisha shukrani,kuna nyakati hutusonga na mambo yanayoleta machozi,kujiona duni au usiye thamani,kuchelewa safari ya mafanikio au hata kupoteza yale uliyohitaji na kuyapa umhimu.Ila haijalishi bado nafasi ipo,kwenye changamoto zozote katu usipoteze T3
•Tumaini
•Tabasamu
•Tegemeo kwa Mungu

    Baada ya sarakasi zoote kwenye jambo lolote
SIMAMA :-hapa weka breki zote,acha pupa,hasira,majuto,acha kutafuta wa kumlaumu au kumtupia lawama,pekua nini kimekufikisha hapo?utakapopata jawabu itakusaidia sana kusonga mbele!

FUTA MACHOZI:-Hapa kabiliana na maumivu yako ya hilo lililokufika si kukwepa au kukataa kwamba umesongwa la hasha hapa kama ni kulia lia wee ila ukiwa umedhamiria kuinuka na kusonga mbele,waweza pata marafiki wema au familia itakayosimama nawe lakini hapa ni kukubaliana na ukweli kwamba mwisho wa siku wewe ndiye rubani wa maisha yako hao wote watapita, maana hata jengo hushikiliwa na machuma wakati wa ujenzi ila baada ya muda uondolewa na jengo hubaki pekee,hapa nina maana kuwa maisha ni WEWE jikung'ute mavumbi na aamua kutoka ndani kusonga mbele!

TAZAMA VYEMA:-Baada ya machozi kufutika naamini macho yataona vyema,zile fursa zilizo mbele yako hapa utagundua pia nini unakikosa kwa kuendelea kukaa kwenye uchungu na kukata tamaa,utaona pia namna unavyopoteza muda kujinung'unikia na kulaumu wengine!Hapa ni kipindi cha kuwa jasiri na kufanya maamuzi yatakayobadili maisha yako kwa mlengo chanya,

Wewe ni shujaa katika lolote unalokabiliana nalo daima jivike jina hili!hili litakupunguzia unyonge na kuwa mtu wa kulialia kila linapotokea gumu na zito

Chukua hatua yote unayotamani yanawezekana hasa na Mungu akiwa upande wako!
Praying for you❤️🙏🏿

Wednesday, January 18, 2017

BEAUTIFUL SINGLE CHRISTIAN GIRLS

BEAUTIFUL SINGLE CHRISTIAN GIRLS!
         Heri ya mwaka mpya warembo!ngoja tufungue mwaka kwa kuongelea hili.

Imekuwa kawaida sana kwa mabinti kupata mafundisho ya kujitunza mpaka ndoa na hasa kutokana na madhara kuwa makubwa na mengi kwa upande wetu!ila kuna katabia kama kanaota mizizi kwa baadhi ya kujitengenezea mazingira ya vijana wa kiume kuwahitaji kingono halafu ikishafika point of no return,mnawaruka kimanga na kuwasingizia kuwa wametaka kuwaangusha dhambini nk. Nk.

Nadhani kama umeamua kujitunza fanya huku ukimlinda na huyo kijana mwenzio ila kumtega naye akanasa, halafu baadaye unatuaminisha kwamba ulilazimishwa nae si sawa!Huwa naamini binti wa kike ndiye mwenye dira ya uhusiano mlionao kama mjitunze mpaka ndoa au la,

Yasome mazingira yanayoongoza mahusiano yenu,msome na yeye madhaifu na nguvu zake (strenghth &weakness) na nyote msaidiane kuifikia NDOA TAKATIFU sio afya sana kuchochea moto usioivisha chochote!

  • Jaribu kurekebisha namna unavyovaa mnapokuwa mnahitaji kuonana,valia kwa staha na si kwa namna ya kutuma ujumbe ambao baadaye utashindwa kuujibu itapobidi kufanya hivyo.
  • Jaribu kuangalia mazingira ya hivyo vikao vyenu vya dharura!
Jifunze tofauti ya kihisia na kibaolojia kati ya wanawake na wanaume juu ya masuala ya tendo la ndoa kwa watu waliokuzidi umri na wenye busara,wakuelekeze kwa utaratibu!Hapa nadhani mnakumbuka vyema hadithi ya Amnoni na Tamari mpaka walivyoanguka katika dhambi!

Ni sawa kuwa binti mwenye misimamo!ila iwe yenye usafi na adabu,sio kumtia kijana wa watu kwenye vishawishi halafu baadaye unamruka!