Thursday, October 19, 2017

Namna bora ya kusubiri

NAMNA BORA YA KUSUBIRI


 Hakuna anayependa KUSUBIRI hasa katika karne hii ya mambo ya shaa shaa/ fasta fasta( A microwaved kinda generation)
Wewe ni shahidi unavyokereka kusubiri foleni bank,taa zinazoruhusu magari barabarani au hata mhudumu anapokucheleweshea chakula/ kinywaji chako!! Kwa Mungu ndio huwa hatumuelewi na tunaumia haswaa!!!pale alichoahidi kinapokawia au unaloomba na kuhitaji kwa sana linapochukua muda kutimia

Kwenye kusubiri suala huwa ni namna gani tunaweza kusubiri na si kama inawezekana/ tunaweza kusubiri!!
Kwenye maisha kuna vingi tunavyohitaji au hata kutamani Mungu atupe lakini haviji paap naongelea zaidi vile unavyoweza kungoja!!
Hutupelekea kumuona Mungu hakuwa in control na haoni uharaka wa hitaji letu!!

Si kipindi kizuri maana
* Moyo huchoka na huumia sana kwani sauti za kujilinganisha na wengine huimba sana!!
* Kujikatisha tamaa au hata kukatishwa tamaa na wengine hujitokeza!!
* Hutufanya tutupe tumaini na tegemeo letu kwa Mungu na hapa ndipo mawazo ya kutafuta njia fupi huja!!

Leo nataka tumtazame Daudi kupitia Zaburi 27 yeye alikuwa ni kijana ambaye alikuwa ametawazwa kuwa mfalme katika umri mdogo sana kama 16 hivi lakini alikutana na mambo magumu mno na iligharimu miaka 14 baadaye ndio akawa mfalme kamili... alipata maadui wa kumtosha alikuwa na mategemeo,matumaini na matarajio kwa Mungu lakini hayakujipa siku moja yalitokea baadae!! Aliumia sana na kulaumu lakini alikuwa na IMANI ipo siku Mungu atabadilisha historia yake na kuleta shwari kuu!!

Mtu mwingine ni Ibrahim nae alipita katika kipindi cha kusubiri baraka yake ya mtoto!!
Ulikuwa ni mtihani kidogo,,huyu ni mtu anayesifiwa kama Baba wa Imani lakini naye alipwaya katika kusubiri. Alifika mahali akaona atafute njia fupi katika kupokea hitaji lake ambalo liliigharimu ndoa yake!

Kusubiri kunachosha na kuna maumivu mengi lakini mara zote Mungu alipochelewesha mambo yetu hulenga
1. kutufundisha uvumilivu na hufunua tabia yetu halisi!!Ni kipindi cha kusubiri baraka za Mungu ndipo utajua tabia yako halisi na hata kujifunza uvumilivu na mengi ambayo Mungu anataka ujifunze kupitia hitaji lako!!
2. Hutufunza namna ya kuweka tegemeo letu kwake na kumtegemea!!
3. kutuandaa kubeba jambo hilo ambalo analiandaa kutupatia, hutusaidia kubeba jambo hilo kwa nidhamu na uthamani kutokana na uzito tuliokuwa nao wakati wa uhitaji nk....
Hapa  nitatoa mfano wangu binafsi kwa miaka zaidi ya 20 nilikuwa na tatizo la sukari ya kushuka na moyo tatizo lililokuwa limenisumbua sana nilikuwa naamini kuna siku nitapona japo kuna saa hali haikuwa inaonyesha nitapona,, Nilipokuwa nikizidiwa na kuona kama leo ndio inakuwa mwisho wa uhai wangu nikawa nasema Mungu utaniponya lini? nachoka kusubiri,,mbona naombea wengine wanapona mie bado? neno lako lina ahadi nyingi mbona hunitendei?nadhani nitakuwa makini na afya yangu maana anytime I can loose it!!
Yeah I got better after waiting for a very looongest time na nikajifunza kuheshimu uhai wangu sana, hivyo kila siku ninapoamka mzima inanipa kuona namna nilivyo si kwa  nguvu au uweza wangu ila ni kwa huruma za Mungu!!Maana yeye ndiye hutoa uzima na anaweza kuchukua muda wowote na nikagundua kule kusubiri kumenipa nidhamu kwa Mungu na kwa jambo alilotenda!!

Sasa ni vizuri kuelewa kila anacholenga Mungu katika jambo unalosubiri maana usipoelewa kila hatua hapo lazima upige maktaimu mpaka mambo yakae sawa ndipo uhitimu na kupokea muujiza wako!!

Kuchelewa kwa jambo lolote jema huwa kumefungwa na ukuu wa kiungu ndani yake sasa likija nusu au bila ukamilifu wake litasumbua tu!! Hivyo ni aheri kusubiri..

  Sijui unasubiri jambo gani naomba nikutie moyo kusubiri katika Mungu!!
Yeye ni mwaminifu sana atatenda kipo anachotaka ujifunze kwake na kipo anachotaka kitendeke ili Yeye atukuzwe kupitia maisha yako VUMILIA

Tutaangalia namna bora sasa ya kusubiri!!
Kwenye sehemu ya mwisho ya somo letu

    Itaendelea........,

No comments:

Post a Comment