Na akaikumbuka thamani yake Part1!!
Mtu yeyote anayeijua thamani yake hujiwekea binafsi viwango vya juu vilivyojaa neema na ustadi katika namna anavyoishi na anavyofanya mambo yake!!
Hakuna anayeweza kuwa vyote kwa kila mtu na kuwafurahisha wote anaokutana nao kwenye maisha lakini anaweza kuujua uthamani wake na kuishi kwa staha akifanikisha mambo yake na kuwa mwenye furaha!!
Ni mpaka tu mtu atakapothamini maisha yake na utu wake ndipo atafikia kilele cha kuwa mwenye furaha na kufanikisha mambo yake pasipo kuwanyooshea wengine vidole kama vicheleweshi au vizuizi vya furaha na kutimiza ndoto zake!!
Jamii nyingi za KiAfrika zimekuwa na mtizamo kandamizi kwa mtoto wa kike/mwanamke kijumla na kadri siku zinavyosogea mambo yanakuwa magumu zaidi hivyo kupelekea wengi kukata tamaa ya kupambania ndoto zao na hata kuishia kuwa wenye huzuni na msongo wa mawazo usiokoma.Sasa kama mwanamke hautaamka binafsi kuitambua thamani yako na kuchangamka tutachelewa sana,maana kila tunapojitahidi kuinuka lazima tuonekane tunatafuta usawa na wanaume au kushindana nao sasa hili si jambo zuri maana tutakuwa na kizazi cha wanawake wanaokalia ndoto na kuwa nyong'onyezi!!
Kama unapita katika hali hizo hebu jaribu kufanya haya:;-
•Linapokuja suala la kuwa na furaha au mafanikio sio sahihi kuweka hisia na matarajio yako kwenye mikono ya mtu mwingine,shauku ya kuwa mwenye furaha au mafanikio inakutegemea wewe binafsi kwa asilimia zote.Imo nguvu ndani ya kila mwanamke ya kuwa bora,kufanya vitu kwa ustadi nk,bila kuitaji maoni ya pili kutoka kwa mtu yeyote na ukilijua hili maisha ni marahisi mno!
1.Angalia ni kitu gani kinakudunisha/kukukwamisha jitenge nacho na ikishindikana kipuuze.Jione kwa namna ambayo Mungu anakutazama kama kiumbe bora na cha maana chenye uwezo wa ajabu kufanya mambo makubwa.
2. Kama uliweka imani yako juu ya watu fulani kwamba bila wao huwezi kuwa mwenye furaha au mafanikio you must take your POWER back si lazima kwa mkupuo anza taratibu kwa kufanya yale yakupayo furaha kibinafsi au vitu vile vilivyo katika uwezo wako kutenda bila mtu wa pembeni.
3. Mwendee Mungu YEYE pekee ndio chanzo cha furaha ya kweli na ndie dira pekee katika kila jambo utakalo kulifanya haijalishi ni kubwa kiasi gani!!Daima yupo kutuonyesha njia
No comments:
Post a Comment