Monday, December 7, 2015

Unalindaje amani yako?

TUNZA NA ILINDE AMANI YAKO!
        ......Just because some people are FUELED by DRAMA doesn't mean you have to attend their PERFORMANCES

Kuna watu furaha yao ni kukuona unapaniki,unalia weee...unakata tamaa..unarudi nyuma..hata kuona unatishia kutoa uhai wako....
Wapo pia ambao hupenda tu kuona unakosa raha au kila wakikutafuta wakiona una furaha,mafanikio,ujasiri watakuchokonoa tu..

            WASHANGAZE!
Ukijua jambo ni ushindi tosha..hi hi hi. WHEN YOU KNOW BETTER..DO BETTER...BE BEST..

Badilisha mbinu..si kila ugomvi lazima uuvalie kibwaya..kuna watu wamebarikiwa ugomvi,chokochoko,husda,vitimbi,chuki,wivu nk.
Ukishaona dalili ya vitu tajwa hapo kwako ni ushindi maana hauna sababu ya kuhudhuria pambano..Wakati mwingine tunapoteza muda,nguvu na hata BARAKA zetu Mungu alizotuandalia kwa kufukuzana na watu kupambana nao au kutayarisha visasi..

Moyo wenye utulivu uliojaa vitu vichache una afya na nafasi ya kufanikisha mipango na mambo mbalimbali..
Akili iliyojaa amani ina afya na uwezo wa kufanikisha vitu lukuki..

Unapojiweka kwenye mazingira ya fujo na vurugu unaharibu afya ya moyo na akili yako,na hutoweza kupiga hatua yoyote kimaisha,kuwa mwenye furaha maana maeneo yote muhimu yamejeruhika.

Pia mwili lazima udhoofike maana kila wakati umekaa kuandaaa mpambano au wakati mwingine hata chakula kwenye koo hakipiti maana moyo na akili vimesongwa mno mno.

INAWEZEKANA KUJILINDA:-kuulinda moyo wako ni kufanya tathmini ya yale yote yanayoujeruhi na kuamua bila hasira wala ugomvi kujitenga mbali nayo.

√Hakiki taratibu watu waliokuzunguka,wana nafasi ipi kwenye maisha yako?ni wenye kukupa afya au nyakati zote ni wa kukutoa machozi na kukurudisha nyuma. Ukijua ni wale wagomvi washari hawa wana nafasi ya kuupata upendo wako wakiwa mbali kwavile wakiwa karibu ni miiba mikali.Usijenge uadui endelea kuwaheshimu na kuwapendaa ila wakiwa mbali.

√Si kila mtu wa kugombana na kujibishana nae.Ukishafahamu kule unataka kufika kwenye maisha yako na ukajitambua wewe ni nani sio afya kupambana na kila mtu..Fanya yale yaliyo ya msingi huku ukizingatia afya ya mwili..moyo na akili yako..

√Wengine ni wa kuwapuuza kwa sisi tunaomuamini Mungu tunaamini  kila mtu aliyeumbwa na Mungu ni mwema ila kuna saa wapo ibilisi ambao huwa anawatumia kuvuruga ndoto za watu,kuharibu amani zao nk. ukijua hili litakupunguzia msongo utapata muda wa kulitathimini jambo kwamba ni flani kweli anafanya hili au shetani ndie ananijaribu kupitia yeye.Ukijua ni shetani usipambane na mtu acha Mungu akupiganie.Kuna baraka zetu zinakuja kutokana na namna tunavyoyakabili mambo.
    Acha wakuone mjinga,legelege lakini kipo unachokitunza..

����Tchao

No comments:

Post a Comment