Tuesday, September 22, 2015

Kwa nini useme ASANTE/THANK YOU

THANK YOU...ASANTE...NASHUKURU

       Ni maneno madogo lakini yenye maana kubwa yakisemwa hasa kwa moyo uliomaanisha...
Huielezea  haiba yako na kukufanya uonekane muungwana na mtu mwenye utu na ubinaadamu pia..
    Kuna mahusiano hujengwa kwa upole,ustaarabu na uungwana pekee..Pengine kwa bahati mbaya tunaishi kwenye karne ya ubize kila mtu anachakarika kutafuta namna atakavyojipatia mahitaji yake makuu matatu ya kila kiumbe hai..Hata hivyooo unafikiri utajisikiaje MTU atakapokupa tabasamu na kukuambia "ASANTE" ..."NASHUKURU"


Kwa wafanyabiashara wanaokwenda nchi za Asia watakwambia umuhimu wa ishara ya kuinama(bow) kila mara wakati wa dili zao,na hata zinapokwenda mrama maana kitendo hicho huwasaidia kwenye mambo yao.

 Na hii ni kama kwa walioko Italia wanavyolipa umhimu neno "GRAZIA MILLE"..

  SHUKRANI
√Hutengeneza nafasi ya kufanyiwa mambo makubwa baadaye na hufungua milango mingi mingi ya mafanikio.
√Huwa ni kiashirio cha kuthamini..kujali..kutambua umuhimu wa tendo au mhusika aliyeshiriki kufanya..
√Hukufanya mtu mwenye furaha..marafiki wengi na mwenye nguvu hii ni kisaikolojia hasa.
***Cha kushangaza si watu wote hutarajia kukufanyia jambo ili urudi kuwashukuru hili ubaki kwako wewe MTENDEWA maana usiposhukuru ni sawa na kuandaa zawadi nzurii..kuifunga kwa nakshi nakshi na kutompa mhusika..inakua haina maana si ndio enhee?.

Unataka kufanikiwa?..kusonga mbele?kuwa mtu wa shukrani kwa Mungu na wanaokuzunguka..umepewa kazi na boss umeikamilisha imekupa pesa nono..rudi mwambie kitu...
√Wewe ni boss waajiri wako wamekutendea kwa uaminifu..Waite. Washukuru uone utendaji kazi na mahusiano yenu kama hayajaimarika..

Unakumbuka nini wakati unakua?ulipopewa kitu halafu hukusema (asante)na vipi uliposema?

Shukuru..shukuru...kwa moyo mweupe kwa kila hali na majira yoyote uliyonayo..

No comments:

Post a Comment