BINTI:-
Jitahidi kuwa HALISI kwenye maisha yako ya mahusiano(love relationship).
Kuna maisha halisi na si kama hayo ya kwenye TAMTHILIA za Telemundo,kiKorea au kiPhilipino.
Kuwa na matarajio ya kati ya kiuhalisia ambayo hata wewe unaweza yafikia na hata yakikawia unaweza vumilia na kusubiri..Kuliko kuwa na matarajio MAKUBWA yatakayozaa NDOA yenye maumivu na majuto..jifunze utofauti wa TAMTHILIA&UHALISIA WA MAISHA..
Pale watu wako kikazi na wanafuata namna mtunzi iwe..pia hata tamaduni zao na zetu ni tofauti.
Mnapokuwa halisi mnafunzana namna ya kujenga mahusiano yenu.
◆mkiwa na fedha muiishije?
◆zikikosekana outing na shopping za Mcity kila wiki?
◆kukiwa na migogoro mtatatua vipi?
Kwenye mapenzi kuna maisha zaidi ya" I love you",kunywa wine. .kushikana mikono huku mnatembea kwenye garden..kwenda swimming pool.
Fanya haya..yakusaidie
★Fahamianeni vya kutosha..mjue huyo kaka na background yake. .huwezi kufahamu yooote siku moja..uliza maswali nk.
★usiwe mwepesi kuvua/vuliwa nguo zako..unless unataka kuchezewa but if you want marriage anayeweka msimamo ni wewe BINTI from day1..
★Ridhika na ulivyonavyo-uwezo wako ni wa kusuka yebo..unataka weaving za Kim Kardashian...ndo msuguano utapoanza na mkaka atakuona upo kimaslahi..let him give it by himself na kumbuka hali yako halisi iishi huku nyingine mnapanga maendeleo maana baada ya no1 utajua tu kama huyu ananioa au anataka Sex tu hapa.
★Jinsi ya kutatua migogoro yenu-hakuna mahusiano ambayo hayakumbwi na mitikisiko..zungumzeni pamoja..chuja watu wa kuwadokeza changamoto zenu si KILA MTU anafaa.
MUNGU anasimama pekee yake mshirikishe katika yote kuanzia mwanzo sema wengi huwa tunamshirikisha vikiharibika.Inua uhusiano wenu mbele za Mungu kila siku na mweleze kila kitu bila kuficha utaona unavoinjoi..
Kumbuka aliyekamilika ni Mungu pekee hata hao waigizaji licha ya kuyapatia mapenzi kwenye TAMTHILIA hizo kwenye maisha yao wanakwama mnooo.
Kipindi cha UHUSIANO ni kipindi cha UNAFIKI alituambia Askofu wetu anapotufungisha ndoa..kwenye NDOA ndio uhalisia unaanza jitokeza.Sasa si vibayaa kuwa makini maaana hapo hulijui jasho la mwenzio maana kila mkimeet mnanukia perfume. .ukikosea unaletewa flowers. .kabla hujamaliza kulalamika umepewa busu na kupokea hela ya saloon..kidogo tuu hela nyingine via m pesa/tigo pesa si ni movie hiyoo jamaniiii? ?????yanawezekana kweli hayo kwa utamaduni wetu wa Ki Tanzania???
Wishing you all the best blessings my girls.
Nawapenda saaana. .
0718664741 let's keep in touch kwa lolote swali au ushauri
No comments:
Post a Comment