Thursday, May 29, 2014

Elimu ni ufunguo wa maisha..na ni ya mhimu usichezee fursa..Kama umeipata

Ukitaja timu ya Mpira wa miguu ya TP Mazembe huwezi kuacha jina la baba huyu almaarufu..Gavana wa jimbo la katanga na mmiliki wa klabu hii Moise Katumbi Chapwe...
Alizaliwa Tarehe 28/12/1964 kama tunavyojua vita vya Kongo na mambo ya hapa na pale alikimbilia Zambia na kurudi Kongo mwaka 2007..Ni mwanasiasa na mfanyabiashara maarufu sana..
Kilichonifanya leo tumzungumzie ni jinsi alivyozungumza kwenye mahojiano yake na kituo cha Supersport japo ilikaa kimpira zaidi ila kuna masuala alizungumza kama gavana na vipaumbele vyake akiwa kwenye utendaji..akasema anachofanya usiku na mchana ni kuhakikisha watu wanapata maisha mazuri na bora..
Alikonikuna haswaaa ni alipozungumza juu ya elimu akasema...

In 2006 we had 600,000 students in primary and secondary schools and now we have 3 million. We have to educate people to give them a chance to do something once the resources disappear. With the help of mining companies, we are training technical people and rehabilitating schools across the province; the DRC needs a middle class. Road infrastructure is also essential: when the Belgians left Katanga, there were only 450 km of roads in a province the size of France. In six years, I have built 1,400 km of asphalt road and 5,000 km of dirt road. A lot of the credit for this goes to the South African IDC bank because they financed a great deal of our development projects. They helped us at the right time because people had nothing to eat and we were importing 90% of our food, while now that number dropped to 35%. I told mining companies to develop agriculture projects because food is a basic need. Without it, people will not be able to do anything and they will look towards their governor to find answers. As a leader, you have to understand the people and not forget them.

Kwa ufupi Bwana Moise alisisitiza kuwa ni kweli Kongo kuna madini lukuki ,,lakini kuna SIKU yataisha hivyo watoto wetu wanahitaji ELIMU ili siku vikipotea na kuisha basi wana kitu cha kuwakomboa ambacho ni elimu!!
Nilipenda mtazamo huu nikajifunza jambo...

Sisi kama waTanzania hatuna hata vita au kufikia mateso wenzetu nchi jirani wanapitia lakini unaiona KIU na MAONO waliyonayo??..nini tunajifunza kama wananchi na hata viongozi..

Jambo hilo mezani kila mtu ajipakulie kulingana na nafasi yake..

√Uko shule tumia fursa uliyonayo vizuri,acha tamaa ya vitu vya njia rahisi au mteremko..Naamini ukitumia fursa hiyo kwa adabu na mipango thabiti ukakumbuka kuna nchi wanalilia nafasi kama yako au kuna vijana wenzako walitamani kuwa hapo ulipo wameshindwa na si kuwa hawana akili la hasha walikosa pesa au sababu zinginezo..Tumia fursa yako vizuri ubadili maisha yako na kuwa msaada wa kwa familia yako,jamii na taifa kwa jumla.
√Kwa uliye kiongozi kipi umekipa kipaumbele..maslahi yako binafsi au kutatua kero za msingi za wananchi?tafakari chukua hatua..

Maisha unayotaka..yapo na yanawezekana...!
Elimu pekee ndiyo urithi pekee kwa kizazi.hiki..
Tutumie fursa tukawape hatua hatua na wengine waliotamani na wakashindwa...
Tanzania kwanza...

No comments:

Post a Comment