Basi weekend hii palee Mbezi Garden Hotel...Tanzania Business Entrepreneurs For Women waliandaa kongamano na maonyesho,ambapo vikundi takribani 30vilionyesha bidhaa zake na washiriki zaidi ya 100 kuhudhuria!!
Fursa za kufunzana jinsi ya kutumia fursa mbalimbali za kimaendeleo na bado kuwa kina mama bora na wa mfano.
!!!
Ilikuwa chini ya Dada HaikaLawere mkurugenzi mtendaji wa Mbezi Garden Hotel,Judith,Beatrice,Naomi nk.
Kulikuwa na mamboo meeengi kutoka ACB bank,Cassandra Lingerie,GS1,TBS ,Paul Mashauri alikuwepo pia na somo la ujasiriamali kutoka kwa Mama Nelly Maliva wa chuo kikuu cha Dar es Salaam(Udbs)...
Kuuubwa kuliko ni wasaa ambao kulikuwa na kipengele cha successful story ambapo mwana mama Maida Ibra Waziri mmiliki wa Ibra contractors Limited..!
Mama huyu alitupa hadithi yake fupi kuwa mara baada ya kumaliza kidato cha nne alianzisha shughuli za ushonaji ambapo alizifanya kwa muda ndipo baadaye akaanzisha kampuni yake ya ujenzi na nyingine wanayotengeneza furnitures..
Ni mwanamke mkandarasi bora kwa mwaka 2011 ..
Alieleza kuwa kila mwanzo hutaka ujasiri na malengo ya dhati kusimamia kile unachotaka kufanya...Na kuwa si lazima mpaka uwe na pesa nyiiingi ndipo uanze wakati mwingine uthubutu uliobebwa na wazo lenye nguvu humfikisha mru mbali..
Anasema changamoto zipo lukuki kama vile mfumo dume,ushindani hasa kwa upande wa contract,mitaji nk. lakini hiyo haimzuii yeye kupenya na kufanikiwa...
Haya sasa kazi kwetu wanawake maana wenzetu wenye uthubutu tumewaona wakipenya na kufanikiwa hiyo itoshe kutupa moyo nasi pia kuwa yote tunayotaka tunaweza kufanya...Tuwe tu majasiri na kutumia nafasi tunazopata...










No comments:
Post a Comment