Si kila changamoto unayopitia inatoka kwa Mungu au shetani anakujaribu..!mmh..!hapana nyingine ni FAULO tu za wanadamu wachache ambao hujiona wao ni Alfa na Omega kwenye maisha ya wengine.!
Kwenye maisha kuna watu hupata fursa ya kuiona baadaye yetu(future) na kwa hofu zao binafsi au chuki huamua kutengeneza mbinu chafu kukudhoofisha usifike mbele au uwe kama wao..!
Usipokuwa na AKILI ya ziada utaumia,utakata tamaa na hata kukimbia kule kwenye furaha ya maisha yako wakati unapaswa ufurahie maisha yako.
Ukisoma KUTOKA1:8-10 pana simulizi ya kutosha juu ya wana wa Israeli walipokuwa utumwani Misri walishamiri na kufanikiwa kuliko wenyeji ikabidi waMisri watumie AKILI ili kuwadhibiti wasiendelee kuwa tishio..
Mambo kama hayo utakutana nayo sana kwenye maisha..jitie moyo ..jivike ujasiri...pambana mpaka kieleweke..
Si tunaona ulaya huko licha ya faulo zote kina Messi,Ronaldo wanafunga magoli tu ya ukweli..
Pambana kila mechi unayokutana nayo na kuchukua pointi za muhimu Away&Home games..
Huku ukinogeesha UHUSIANO WAKO NA MUNGU..
watashindana sawa..wanaruhusiwa 24//7 ila kushinda ndo ngumu maana Mungu yuko upande wako...
kisses and blessings to y'all
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment